• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Geita Aipa Joto la Ushindi Timu ya Geita Gold FC Dhidi ya Pamba Sports Club ya Mwanza, Asema ana Deni Kwao.

Posted on: November 20th, 2020

Ikiwa yamesalia masaa kadhaa kuelekea mtanange mkali unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza Novemba 21, 2020 kuanzia saa kumi jioni baina ya timu ya Geita Gold FC kutoka Geita inayomilikiwa na halmashauri ya mji Geita na timu ya Pamba FC ya Mwanza, mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel leo Novemba 20, 2020 amefika ilipo kambi ya wachezaji wa timu hiyo ya Geita zilipo nyumba za NHC eneo la Magogo kwa lengo la kuwatia moyo na hamasa ili waweze kuwa washindi wa mchezo huo.

Akizingumza na wachezaji pamoja na viongozi wa timu hiyo, mhandisi Gabriel ameeleza kuwa, kupitia sura ya 242 hadi 243, ukurasa na. 291 hadi 294 wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, tayari serikali ilielekezwa kuendeleza na kusimamia michezo katika ngazi mbalimbali nchini, hivyo kama kiongozi mkuu wa serikali mkoani geita, atahakikisha anatekeleza wajibu huo kama maelekezo yalivyotolewa.

“niwapongeze kwakuwa mmeanza vizuri na kiu yangu ni kuona maisha yenu yanaenda mbali zaidi. Ifike mahali ukiwa uwanjani usipoteze mpira kwakuwa unajua una wajibu mkiyajenga maisha yenu kupitia mpira na kama kiongozi tunaanza na utafutaji wa kiwanja kwaajili ya kocha kisha wachezaji mtafuata, hii yote ni katika kuhakikisha mpira unakuwa ni sehemu ya maisha yenu. Hivyo jueni mna deni kuutangaza mkoa nasi tuna deni kuwainua”, mhandisi Gabriel alieleza.

Pia, mkuu wa mkoa huyo alilisisitiza juu ya kuwa na tabia ya kuwekeza ikiwa tunataka matokeo mazuri huku akieleza kwa ufupi wasifu wa kocha wa sasa wa timu ya Geita Gold ndg. Fredy Minziro, kisha kumpigia simu mkuu wa wilaya ya geita ili aambatane na timu hiyo siku ya jumamosi ya Novemba 21, 2020 kwaniaba ya serikali ya mkoa katika mtanange huo.

Katika hatua nyingine, kocha wa timu hiyo ndg.Fredy Minziro alimshukuru mhandisi Gabriel kwa kuwatembelea na kuwatia moyo huku akiahidi ushindi wa kishindo akisema anaamini ushirikiano wanaoupata kutoka serikalini na kwa wadau mbalimbali utaisababisha timu hiyo kusonga mbele.

Akishukuru kwaniaba ya timu, nahodha Joseph Mwarabu alishukuru ujio wa RC Geita na kumsihi asiichoke timu hiyo na kwamba wanaamini watatimiza malengo yao ikiwemo ya kupanda daraja.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Geita Gold Fc ya Geita kuchuana na timu ya Pamba FC ya Mwanza ili kuingia ligi kuu.



Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka -2021, Mkoa wa Geita. December 18, 2020
  • Fomu ya Ushiriki Kwenye Maonesho ya Tenkolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mjini Geita August 06, 2019
  • Vigezo vya Udhamini, Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita August 06, 2019
  • Matokeo Darasa la Nne Mkoa wa Geita January 11, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Robert Gabriel aagiza kukamatwa kwa Mtendaji wa Kijiji aliyetoroka na fedha za Michango ya Madawati

    February 03, 2021
  • RC Geita Aipa Joto la Ushindi Timu ya Geita Gold FC Dhidi ya Pamba Sports Club ya Mwanza, Asema ana Deni Kwao.

    November 20, 2020
  • "Walimu na CWT, Tuisaidie Jamii Ijue Tulipotoka, Tulipo na Tunapokwenda" RC Geita Anena Hayo

    October 17, 2020
  • Wataalam wa Ardhi Watega Sikio Kupata Tafsiri ya Ardhi Waliyonayo Wananchi Mkoani Geita

    October 17, 2020
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: Box 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa