Mtandao wa Barabara chini ya Usimamizi wa TANROAD
Mkoa una mtandao wa barabara unaosimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoani Geita. Mtandao huu una jumla ya kilomita 848.46. Kati ya hizo barabara kuu (trunk roads) ni kilomita 236.18 na barabara za mkoa (regional roads) ni kilomita 612.28. Aidha, Barabara za kiwango cha lami ni kilomita 396.66 (46%) ya mtandao wote ambapo barabara kuu ni kilomita 236.18 (100% ya Barabara Kuu) na za mkoa ni kilomita 160.96 (26% ya Barabara za Mkoa).
TANROADS Geita inasimamia barabara za halmashauri za wilaya zenye urefu wa kilomita 78.87 ambazo zimekasimishwa kwa muda. Kati ya hizo kilomita 2.66 ni za lami na zilizobaki kilomita 76.21 ni za changarawe.
Hali ya barabara za mkoa ni nzuri na zinapitika vipindi virefu vya mwaka kutokana na ukarabati na matengenezo ya aina mbalimbali yanayofanyika. Barabara za lami ni kilomita 160.96 (26%) na zilizobaki kilomita 451.80 ni za changarawe/udongo.
Mtandao wa Barabara chini ya Usimamizi wa TARURA
Wakala wa Barabara (TARURA) Mkoa wa Geita anasimamia barabara zenye urefu wa Kilomita 7,263.55, barabara za Wilaya (Collector Roads) ni kilomita 2894.33(39.85%), barabara za Jamii (Community Roads) ni kilomita 730.48 (10.06%) na kilomita 3638.74(50.09%) ni barabara Ndogo (Feeder Roads). Barabara za lami ni kilomita 44.98(0.62%), barabara za changarawe ni kilomita 1,986.77(27.35%) na barabara za udongo ni kilomita 5,231.79(72.03%).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa