Huduma ya Maji – Vijijini
Mkoa wa Geita una jumla ya vijiji 486 ambapo kati ya hivyo vijiji 354 vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama ambapo hupatikanaji wa maji ni lita za ujazo 32,040,705 kwa siku kwa wakazi wanaokadiriwa kufikia 1,408,006 sawa na asilimia 66% ya mahitaji ya lita za ujazo 53,401,175 kwa wakazi wanaokadiriwa 2,136,047 upatikanaji wa maji vijijini. Aidha vijiji 132 bado havijafikiwa na huduma hiyo. upatikanaji wa maji huo umetokana na miradi ya maji ya skimu ya bomba (44), visima virefu vilivyofungwa pampu za mkono (362), visima vifupi vilivyofunga pampu za mkono (794) kwa wa kazi wote wanaoishi vijijini.
Uboreshaji wa Huduma ya Maji Safi na Salama Vijijini.
Hali ya upatikanaji wa maji safi na salama vijijini ni wastani wa asilimia 53%. Aidha, miradi mbalimbali ya maji inaendelea kutekelezwa kwa lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa huduma za maji vijijini ili kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana na kukidhi malengo yaliyowekwa ya kufikia asilimia 85 ifikapo 2025.
Usimamizi na Uendelezaji wa Miradi ya Maji
Katika suala zima la usimamizi na uendelezaji wa miradi ya maji, Mkoa wa Geita umeendelea na zoezi la Umarishaji na uhuishaji wa Jumuiya za Usimamizi wa huduma za maji ngazi ya jamii (Community Based Water Supply Organization - CBWSOs) kwa mujibu wa Sheria mpya na. 05 ya mwaka, 2019. Hadi kufikia Desemba, 2021 jumla ya CBWSOs 57 zimeundwa kwenye maeneo ya miradi ya maji katika Wilaya tano (5) za Mkoa wa Geita ili ziweze kusimamia miradi hii kwenye maeneo ya
Mahitaji ya huduma ya maji kwa wa kazi waishio katika miji ya Mkoa wa Geita ambayo ni Geita Mjini, Ushirombo na Chato ni wastani wa lita za ujazo 25,086,180 kwa siku kwa wakazi wanaokadiriwa kufikia 358,374 wanaoishi maeneo ya mijini, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa sasa ni wastani wa lita 16,306,017 kwa siku sawa na 69% ya mahitaji ya maji, ikiwa ni wastani waongezeko la asilimia saba (7%) kutoka Desemba, 2021
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa