SEKTA YA MIFUGO
Mkoa wa Geita ni miongoni mwa Mikoa nchini yenye idadi kubwa ya mifugo. Mkoa unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 1,118,585, mbuzi 497,774, kondoo 106,336, nguruwe 14,405 na kuku 3,191,554. Mazao makuu ya mifugo yanayozalishwa ni nyama na maziwa. Mazao mengine ni ngozi, mayai na mbolea aina ya samadi.
Mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya Mifugo
Mkakati wa mkoa katika sekta ya mifugo umejikita katika Kuboresha miundombinu ya Mifugo, Kudhibiti magonjwa ya mifugo na Kuhamasisha ufugaji bora.
Ili kutekeleza mikakati hiyo; Mkoa unaendelea kuzisimamia Halmashauri katika kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa Machinjio ya kisasa katika Halmashauri ya Mji wa Geita eneo la mpomvu ambapo mradi huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 150 kwa siku sawa na wastani wa ng’ombe 4,500 kwa mwezi. Hivyo, mpaka kukamilika kwa machinjio zote Mkoa utakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 79,200 kwa mwaka.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza mchakato wa ujenzi wa miundombinu ya mnada mkubwa wa upili (Secondary Market) Wilayani Chato. Mpaka sasa Mkandarasi (Shirika la Nyumba la Taifa), anaendelea na ujenzi. Hata hivyo, katika kipindi cha 2018-2020 Halmashauri zimejenga na kukarabati jumla ya majosho 29 kati ya majosho 57. Hii ni hatua kubwa inayochukuliwa na Serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya Mifugo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa