Historia ya Mkoa wa Geita
Mkoa wa Geita ulianzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 02 Machi, 2012, na kuzinduliwa tarehe 08, Novemba, 2013 na Mheshimiwa DKT Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkoa huu ulitokana na sehemu ya Mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga ambapo upande wa Magharibi na Kusini unapakana na Mkoa wa Kagera, upande wa Kusini na Kusini Mashariki unapakana na Mkoa wa Shinyanga na Mwanza kwa upande wa Kaskazini unapakana na Ziwa Victoria.
Umbile la Mkoa na Maeneo ya Utawala
Mkoa huu una eneo au ukubwa wa kilometa za mraba 21,879 (Geita 6,375 km2, Bukombe 6,798 km2, Chato 3,572 km2, Mbogwe 3,684 km2, na Nyang`hwale 1,450 km2), kati ya hizo kilomita za mraba 19,933 niza nchi kavu na kilomita za mraba1,946 ni za maji.
Mkoa una Wilaya tano (5), Majimbo saba (7) ya Uchaguzi, Halmashauri sita (6), Mji mdogo 1, Tarafa23, Kata 122, Vijiji 474, Vitongoji 2,219 na Mitaa 65. Wilaya hizo ni Geita, Nyang‟hwale,Chato, Bukombe na Mbogwe.
Mkoa una jumuisha Halmashauri ya Mji Geita, Halmashauriza Wilaya za Geita, Nyang’hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Kuanzishwa kwa Mkoa huu kumesaidia kuharakisha upelekaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na maendeleo kwa wananchi.
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa una wakazi wapatao 2,977,608 ambapo wanaume ni 1,463,764 na wanawake ni 1,513,844
.
Idadi ya Watu Kiwilaya kwa Mwaka 2012
Wilaya
|
Jumla ya Wakazi
|
ME
|
KE
|
Wastani watu kwa Kaya
|
Uwiano wa jinsia
|
Geita
|
807,619
|
400,475
|
407,144
|
5.9
|
98
|
Bukombe
|
224,542
|
110,857
|
113,685
|
5.9
|
98
|
Chato
|
365,127
|
181,365
|
183,759
|
6.0
|
99
|
Mbogwe
|
193,922
|
65,083
|
98,839
|
6.4
|
96
|
Nyang`hwale
|
148,320
|
73,272
|
75,048
|
6.8
|
98
|
Jumla
|
1,739,530
|
861,055
|
878,475
|
6.1
|
98
|
Chanzo: NBS, 2012
Hali yaHewa
Mkoa unapata mvua za kutosha kuanzia milimita 900 hadi 1200 na joto la wastani la nyuzi 22 hadi 30 kwa mwaka. Aidha, Mkoa umekuwa ukipata mvua za vuli katika kipindi cha kuanzia Septemba hadi Desemba na mvua za masika kuanzia mwishoni mwa mwezi Februari hadi Mei. Pia, kipindi cha kiangazi huanza mwanzoni mwa mwezi Juni hadi Septemba kila mwaka na unyevu wa kati ya asilimia 35 na 60.
Shughuli Za Kiuchumi na Pato la Mkoa
Wakazi wa Mkoa wa Geita wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji wa mifugo mbalimbali na nyuki, uvuvi, uchimbaji madini pamoja na biashara ndogo ndogo. Aidha, Sekta ya kilimo ina changia takribani asilimia 70 ya pato la Mkoa wa kati shughuli nyingine za kiuchumi zinachangia asilimia 30. Kwa mujibu wa takwimu kutoka NBS mwaka 2013 zinaonesha kuwa mchango wa Mkoa wa Geita katika pato la taifa umefikia shilingi bilioni 1,584 wakati Pato la mwananchi ni Shilingi 910,824.
Fursa za Uwekezaji zilizopo Mkoani Geita
Mkoa unafanya vizuri katika Uwekezaji na una zitangaza fursa mbali mbali zilizopo. Fursaza Uwekezaji katika Mkoa zipo katika Sekta za:- Kilimo, mifugo, madini, uvuvi, ujenzi, misitu na utalii. Pia hupatikana katika Sekta za Usafirishaji na Nishati. Mkoa unafanya jitihada mbalimbali za kuvutia wawekezaji na kuzinadi fursa za uwekezaji zilizopo ili wawekezaji waje kuwekeza na hatimaye kuongeza kasi ya maendeleo ya Mkoa. Baadhi ya wawekezaji ni Ukurwa Investments, Lake Gas, Lenny Hotel Limited, Waja Schools & Hospital, Makoye Hospital, Chobo Investiment, National Housing Cooperation, GGM na VETA.
Orodha ya Viongozi wa Mkoa wa Geita toka Kuanzishwa Kwake Mwaka 2012
1. Wakuu Wa Mikoa
NA.
|
JINA
|
CHEO
|
MWAKA
|
1.
|
Mhe. Magalula Said Magalula
|
Mkuu wa Mkoa
|
2012-2014
|
2.
|
Mhe. Fatma A. Mwassa
|
Mkuu wa Mkoa
|
2014-2016
|
3.
|
Mhe. Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga
|
Mkuu wa Mkoa
|
2016-2017
|
4.
|
Mhe. Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi
|
Mkuu wa Mkoa
|
2017-2020
|
5.
|
Mhe. Rosemary Staki Senyamule
|
Mkuu wa Mkoa
|
2020-2022
|
6
|
Mhe. Martine Shigela
|
Mkuu wa Mkoa
|
2022
|
2.Makatibu Tawala wa Mkoa
NA.
|
JINA
|
CHEO
|
MWAKA
|
1.
|
Ndugu. Severine Kahitwa
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2012-2014
|
2.
|
Ndugu.Charles A. Pallangyo
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2014- 2016
|
3.
|
Ndugu.Selestine M. Gesimba
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2016-2018
|
4.
|
Ndugu. Denis I. Bandisa
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2018-2020
|
5.
|
Ndugu. Mussa Chogero
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2020-2022
|
6.
|
Prof.Godius Walter Kahyarara
|
Katibu Tawala Mkoa
|
2022-
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa