Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe.Rosemary Senyamule ameonesha kutoridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Geita-RVTC kisha kutoa maagizo na kuwaelekeza wanaotekeleza ujenzi wa mradi huo kutokuwa na tabia ya kujiongezea muda wa utekelezaji tofauti na maelekezo ya serikali.
Hayo yamejili Mei 19, 2022 wakati mhe.Senyamule alipotembelea eneo la Magogo unapoendelea ujenzi wa chuo hicho akiwataka mafundi kufanya kazi zinazoendana kwa wakati mmoja na si kusubiri, ili kiu ya serikali na wananchi wa Geita ya kuanza kutumia chuo hicho itimie ukizingatia awali mkandarasi aliyekuwepo alishindwa kutekeleza hadi kuvunjiwa mkataba.
“tunamshukuru mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwani aliona Geita bado tunastahili kupata chuo hiki na ndiyo maana kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 aliidhinisha Bilioni 4.2 ili chuo hiki kiweze kujengwa. Lakini mshauri elekezi utambue kuwa, hatutakubali Tanzania icheleweshewe fedha kwasababu ya kuchelewa kwa mradi huu. Fanyeni juu chini, usiku na mchana mradi huu ukamilike ifikapo tarehe 20 Juni, 2022”. Alisema Mhe.Senyamule.
Aliongeza kuwa, “niwaelekeze pia kuzingatia maoni na ushauri wa wataalamu uliotolewa na mtambue kuwa, mradi huu ni wa wananchi hivyo mnapaswa muwasilishe taarifa ya maendeleo ya mradi kila ijumaa. Mwisho anayehusika na ujenzi wa nguzo za vyuma ahakikishe anafika ofisini ili kutoa maelezo ya ukalimishaji wa sehemu inayomhusu”
Nao (mtendaji mkuu pamoja wataalam) kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita ndg. Herman Matemu ambaye ni kaimu katibu tawala mkoa, Ndg. Salome Cherehani, Ngd.Deodatus Kayango pamoja na mhandisi Rose Mbai kwa nyakati tofauti kila mmoja alieleza namna uhaba wa mafundi umepelekea kuchelewa kwa kazi hiyo licha ya changamoto aliyoitaja mshauri elekezi na hivyo kushauri iongezwe nguvukazi.
Awali akisoma taarifa ya mradi, mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Sengerema ndg.Hagai Shilah ambao hutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) alisema ujenzi wa chuo hicho unatekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 4.2 na kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 320 wa bweni badala ya wanafunzi 88 wa awali na kuiwezesha serikali kuokoa zaidi ya Bilioni 4 ambazo ilikuwa izitumie awali kupitia mkandarasi kwani sasa hutumika njia ya “force account” ujenzi wa kutumia mafundi.
Mradi wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi – VETA Geita – RVTC una jumla ya majengo 26 na kati ya hayo zipo karakana 11 zikiwemo za umeme wa magari na ile ya ukarimu, TEHAMA, nyumba ya mkuu wa chuo, madarasa, mabweni, jiko ukumbi n.k ambavyo vyote hutimiza asilimia 51 ya ujenzi hadi hivi sasa.
Hata hivyo, ngd. John Idelya kutoka chuo cha ufundi Arusha kwaniaba ya mshauri mwelekezi aliahidi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha chuuo hicho kinakamlika na kwamba watatekeleza maagizo ya mkuu wa mkoa aliyoyatoa.
Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima. Kazi Iendeleee
Imeandaliwa na
Boazi Mazigo
Ag.HGCU
Geita RS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa