Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Martine Shigela ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli katika Mkoa wa Geita.
Mhe. Shigela ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akitembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbli inayoendelea katika Wilaya ya Chato mkoani Geita pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara kwa lengo la kusikiliza kero zinazowasumbua na kutafuta namna ya kuzitatua.
Akitembelea majengo ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha Kampasi ya Geita ,Mkuu wa Mkoa wa Geita ametoa wito kwa wanafunzi wenye sifa walioko Geita na mikoa ya jirani kutohangaika kusafiri kufuata elimu mbali bali wajiunge na Chuo cha IFM tawi la Geita ambapo udahili wa wanafunzi kuanzia mwaka huu wa masomo 2024/2025 umeanza. Pia amewakumbusha wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara kama maduka, hoteli, migahawa, stationary nk zitakazopatikana chuoni hapo baada ya kufunguliwa.
Akikagua ujenzi wa Hoteli ya nyota tatu Burigi-Chato, Mhe. Shigela ametoa pongezi kwa Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kufikisha asilimia 70% ya ujenzi na kutoa ombi kwa TANAPA kutoa fedha kwa wakati ili ujenzi wa hoteli hiyo uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma zitakazowezesha kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa, kuondoa changamoto ya malezi kwa wageni, kutoa fursa ya ajira kwa wananchi na kukuza uchumi wa Wilaya ya Chato na Mkoa wa Geita kwa ujumla kupitia sekta ya utalii.
Mbunge wa jimbo la Chato Mhe. Medard Kalemani ametoa ombi kwa uongozi wa TANAPA kuwapatia kipaumbele cha ajira za kudumu wakazi wa wilaya ya Chato mradi huo utakapoanza kazi ili mwananchi mmoja mmoja aweze kujipatia maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita amemshuru pia Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha ujenzi wa Mataba ya kisasa ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa katika kanda ya ziwa na kutoa agizo kuwa Maktaba hiyo itakapokamilika itumiwe na watu wa rika zote.
Mhe. Shigela ameeleza wananchi kuwa changamoto ya uhaba wa maji itafika mwisho baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji katika kata ya Bukome wilayani Chato ikiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa katika miji 28 Tanzania kwa shilingi Bilioni 38.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa