Katibu Tawala Mkoa wa Geita Ndg.Mohamed Gombati amesema kuwa Bonanza la watumishi hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali na Kudumisha Afya ya akili sambamba na kujenga ushirikiano imara Mkoani Geita.
Akizungumza na wanamichezo kutoka Taasisi mbalimbali za Umma Katika Viwanja Vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu Tarehe 26Julai 2025 Ndg.Mohamed Gombati, amesema Mabonanza ya watumishi yanaongeza mshikamono,urafiki na ushirikiano na kudumisha afya ya akili kwa watumishi na kutoa huduma iliyobora kwa wananchi.
Katibu Tawala Mkoa wa Geita amewasisitiza watumishi wa umma kufanya mazoezi na kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na Geita jogging Club kuhudhuria mazoezi ya mbio za taratibu(jogging) kila jumamosi Geita Mjini.
Ndg.Mohamed Gombati amezipongeza Taasisi zilizoshinda Michezo mbalimbali ikiwemo urushaji wa tufe,mchezo wa bao, mchezo wa mpira wa miguu,kuvuta kamba,kucheza mziki,mchezo wa kula,urushaji wa mkuki kwa kutoa medali na vikombe kwa washindi wote.
Aidha ameongeza kuwa Bonanza la mwisho wa mwaka litafanyika mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili na Amesisitiza taasisi zote ziendelee kufanya maandalizi ya Bonanza hilo kubwa.
Kwa upande wa washindi, mshindi wa mchezo wa wavu ni timu ya Manispaa ya Geita,mshindi wa kikapu ni Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kuvuta kamba mshindi ni timu ya Geita-Rs ya wanawake,mshindi wa kamba wanaume ni taasisi ya Tume ya madini,Mshindi wa Mpira wa mpira wa miguu ni Halmashauri ya Wilaya ya Chato, na Mshindi wa jumla ni halmashauri ya wilaya ya Geita.
Bonanza la watumishi linaongozwa na kauli mbiu isemayo "Michezo kwa Watumishi Afya Bora Ushirikiano thabiti,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa