RC Geita Mhe.Rosemary Senyamule Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Kufuatia Kupata Hati Inayoridhisha Mwaka wa Fedha 2020/21.
Hayo Yameelezwa Leo Juni 22, 2022 Wakati Akiongoza Kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Huku Akisisitiza Juu ya Mambo Mbalimbali Ikiwemo Kuwachukulia Hatua Watumishi Wanaosababisha Hoja kwa Uzembe au Sababu Zisizo za Msingi.
"Niwapongeze WanaBukombe kwa Kupata Hati Safi, Hadi Nimetamani Matokeo Haya Yawe Hivi Hivi Siku Zote na Hata kwa Mkoa Mzima. Lakini Pia Niwapongeze kwa Kuvuka Lengo la Ukusanyaji Mapato kwa Mwaka 2021/22 kwa Kukusanya Asilimia 100.03 Hadi Kufikia Juni 19, 2022" Amesema Mhe. Senyamule
Pia Mhe.Senyamule Ameongeza Kuwa "Ninakemea Uzembe Utokanao na Baadhi ya Watumishi Wazembe Ambao Husababisha Hoja Zisizo za Lazima na Ninaagiza Wachukuliwe Hatua. Pia Ninazielekeza Halmashauri Kupeleka Fedha za Makusanyo Benki Kabla ya Kuzitumia"
Amesema, "Nirudie Kuagiza Kuwa, Kamati ya Ukaguzi Yapaswa Kukaa Kila Robo ili Kupunguza na Kumaliza Hoja. Aidha kwa Upande Mwingine, Kamati ya Fedha ni Vyema Nanyi Muifanye Agenda ya Hoja Kuwa ya Kudumu Kwenye Vikao Vyenu".
Kupitia Kikao Hicho Mhe.Senyamule Ameziagiza Halmashauri Zote Kumaliza Miradi ya Pamoja kwa Wakati Kama ya SEQUIP na Kuwataka Watumishi Kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Serikali.
Aliongezea Kuwa "Madiwani Niwaombe Tuisemee Serikali ili Wananchi Wajue ni Nini Inafanya Kwani Tukikaa Kimya Tutakuwa Hatuwatendei Haki Wananchi na Serikali"
Akimaliza Kabla ya Kuahirishwa Kikao, RC Senyamule Alikumbusha Juu ya Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi Akiwataka Viongozi Kuwaelimisha Wananchi Juu ya Umuhimu wa Kushiriki Zoezi Hilo Muhumu na pia Kujiandaa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Akisema Kuwa Ofisi ya Mkoa Itaendelea Kutoa Ushirikiano na Iko Tayari Kushirikiana Nao ili Kutimiza Ndoto Kubwa za Mkoa.
Awali, Mkaguzi Mkuu wa Nje (M) Geita CPA Richson Ringo Baada ya Kuwasilisha Taarifa Yake, Aliwashukuru Bukombe DC kwa Ushirikiano na Kuwakumbusha Watumishi na Viongozi Kuzingatia Taratibu, Miongozo na Sheria Mbalimbali ili Kuupunguza Uwezekano wa Hoja.
Kwa Upande Mwingine, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe.Said Nkumba Amesema Anawashukuru na Kuwapongeza Mkurugenzi, Wataalam Pamoja na Madiwani kwa Kazi Nzuri Waliyoifanya ya Kukusanya Mapato Lakini Pia Kusema Kuwa Wapo Tayari Kudhibiti Mambo Yanayopelekea Hoja
Naye Bi.Sania Mwangakala, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Amesema Ukusanyaji wa Mapato, Upelekaji 40% ya Mapato ya Ndani Kwenye Miradi ya Maendeleo, Kutoa Mikopo ya 10% ya Mapato ya Ndani kwa Kundi la Vijana, Wanawake na Wenye Ulemavu, Lakini Pia Kufuatilia Marejesho ya Mikopo Hiyo ni Vigezo Ambavyo Vinatumika na Ofisi ya Rais-TAMISEMI Kupima Utendaji wa Halmashauri Hivyo ni Muhimu Kuendelea Kuvizingatia.
Mwangakala Vilevile Amewasihi Wakurugenzi Kuwapeleka Mafunzo Wahasibu Ili Kuongeza Ujuzi Kwani Viwango vya Kimataifa vya Ufungaji wa Hesabu Vinabadilika na Kwa Kufanya Hivyo Itaongeza Ufanisi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukombe Mhe.Daniel Machongo Amewaeleza Watumishi wa Bukombe DC Kuendelea Kutimiza Majukumu Yao na Wapunguze Hoja za Ukaguzi ili Serikali Iendelee Kuleta Fedha Nyingi na si Vinginevyo.
Akitoa Neno la Shukrani, Mkurugenzi Mtendaji Bw.Lutengano Mwalwiba Amesema "Tunataka Kuwa Shamba Darasa la Nchi Katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM" Akimaanisha Kuwa Wataendelea Kuhakikisha Wanaepuka Hoja Zisizo Msingi na Kwamba Watazingatia Maelekezo Yote Yaliyotolewa na Mhe.Mkuu wa Mkoa Pamoja na Wataalam Kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Nje
Boazi Mazigo
Ag.HGCU
Juni 22, 2022
Bukombe-Geita
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa