Tangu mwaka 2019 uanze, Mkoa wa Geita umekua na ndoto kadhaa katika kufanikisha kuwa, madini ya dhahabu inayozalishwa ndani ya mkoa huu inaleta matokeo chanya jambo linalopelekea Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Eng. Robert Gabriel Kuhamasisha uanzishwaji masoko ya madini ambayo kwa Geita hadi sasa yapo sita.
Naomba kukurudisha nyuma kidogo hadi mwezi Februari mwaka huu 2019.
Ni bahati iliyoje, tarehe 25.02.2019, Mwekezaji na Mtanzania Mama Sarah Masasi alifika Mkoani Geita kwa mara ya kwanza na kwa lengo la kuwekeza katika sekta ya madini hususan ya Dhahabu kwa kudhamiria kuweka mtambo wa Uongezaji Ubora Madini ya Dhahabu huku akipokelewa na wenyeji mkoani hapa wakiongozwa na Mhe.Eng.Robert Gabriel.
Baada ya kupokelewa na timu iliyosheheni wataalam kutoka katika mnyororo mzima wa kufanikisha uanzishwaji wa kiwanda wakiwemo wa TANESCO, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, TARURA n.k, Mama Masasi ambayr ni mwekezaji aliesema amefarijika sana kwa mapokezi hayo akiamini uwepo wa timu hiyo utapelekea mafanikio makubwa kwake katika kuanzisha shughuli hiyo muhimu.
Alisema, “mimi ni mtendaji na mtekelezaji nisingependa kusema maneno mengi kwakuwa nimekuwa nikishughulikia jambo hili tangu miaka minne iliyopita, baada ya serikali kuhamasisha ujenzi wa viwanda hivi, na Eng. Gabriel pia, hatimaye leo nimefika, nashukuru sana RC na watu wako. Ningependa kuhakikishiwa kupata eneo la ukubwa wa heka 4.5 likiwa mahali salama lakini vile vile malighafi isiyopungua tani hamsini hadi themanini kwa mwaka”.
Mama Masasi aliendelea kusema kuwa, mitambo itakayotumika itawekwa na Kampuni ya Kimataifa ya Bactrac Company Technologies TERA inyoaminika duniani ambayo pia ina uwezo wa kutenganisha madini ya dhahabu na madini ambatana, hivyo akasema angependa kuhakikishiwa uwepo wa mazingira mazuri kiuwekezaji baina ya pande zote yani Serikali, Mwekezaji na Wateja wa Dhahabu
Mama Masasi alimaliza kwa kusema, “ninasema kwa nia moja, asante Mungu kunifikisha hapa na kufahamiana na nanyi, ninaahidi kuwa mtumishi wenu nikihakikisha Geita inafahamika kimataifa kwa uzalishaji Dhahabu na mjue ninawahitaji kila siku ya maisha ya mradi huu”
Kwa Upande wake Mkuu wa MKoa wa Geita Mhe.Eng. Robert Gabriel alimweleza mwekezaji huyo kuwa, hakukosea kuja Geita na kisha kumhakikishia upatikanaji wa eneo la ukubwa wa heka 5 bure tofauti na maombi yake ya heka 4.5, pamoja na kumhakikishia usalama na upatikanaji wa malighafi dhahabu, huku akimhakikishia uwepo wa miundombinu yote itakayotosheleza uanzishwaji wa kiwanda hicho kisha kuambatana na ugeni wake kuelekea eneo litakapofunguliwa soko la dhahabu Mjni Geita na baadaye kwenye eneo la uwekezaji litakalojengwa kituo cha uwekezaji mkoani hapa.
Naye Bw. Charles Itembe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Azania Bank alisema, wao kama mkopeshaji wa mwekezaji huyo wangefurahi kuona anapata uhakika wa malighafi ili aweze kurudhisha mkopo kutoka benki yao na kwamba anaamini kutakuwa na akiba ya kutosha ya dhahabu.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita Dkt.Japhet Simeo kwa upande wake akawashauri watalaamu wa madini kuwa, ni vyema kuwa na taarifa kamili na sahihi ili kuepuka kumvunja moyo mwekezaji na kwamba taarifa atakazozipata zitamwezesha kuamua ni aina gani ya uwekezaji anaweza kuufanya.
Mwisho, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita Bw. Daniel Mapunda akamtoa hofu lakini kuomba muda ili kuja na takwimu sahihi zitakazoweza kumhakikishia na kumpa ujasiri mwekezaji huyo kuhusu upatikanaji malighafi huku akimwelekeza taratibu za kufuata akimsisitiza kuzingatia kipengele cha mahusiano kwa jamii itakayomzunguka lakini vilevile ajira kwa wazawa.
Hivyo basi, kwa mara nyingie Agosti 29, 2019, Mama Sarah aliwasili Geita na kupokelewa kisha kupelekwa kwenye eneo atakalojenga mtambo wa Uongezaji Ubora Madini ya Dhahabu ambapo kama ilivyo sera ya mkoa huu wa kutokuwa na urasimu, Mama Sarah Amepewa Kiwanja chenye Ukubwa wa Ekari nane Bure kilichopo Mtaa wa Bombambili, Kata ya Bombambili, pamoja na hati kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mji geita japokuwa awali alitaka ekari tano.
Haikuishia hapo, bali ofisi hiyo ya Mkurugenzi wa Mji Geita tayari imechonga barabara yenye urefu wa Km. 3.5 kufikia eneo la mwekezaji huyo, ambapo TANESCO na Mamlaka ya Maji ya GEUWASA wako kwenye taratibu za kufikisha miundombinu hiyo.
Baada ya kuoneshwa eneo hili lililopo maeneo ya viwanda, Mama S
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa