Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel Ameupongeza Mgodi wa Dhahabu Geita GGML kutokana utekelezaji mzuri wa miradi ndani ya Halmashauri ya mji geita kupitia fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii yaani CSR.
Ametoa pongezi hizo Aprili 23, 2021 wakati wa ziara yake kwenye miradi ya elimu na afya katika Halmashauri ya mji geita ikiwa ni Halmashauri ya Mwisho kutembelewa katika ziara iliyohusisha majimbo yote ya Geita ndani ya wilaya 5.
Amesema, " niwapongeze GGML kwa jinsi mnavyoshirikiana na serikali pamoja na wanachi katika kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkalanga kwa asilimia 100, hongereni sana. Vilevile, nipongeze uongozi wote kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya, CCM, Diwani, Mkurugenzi mpaka mtaa kwa hatua za utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, mabweni, vyoo pamoja na nyumba za watumishi"
Aidha, mhandisi Gabriel ameendelea kusisitiza juu ya kutokomeza madaraja 0 na IV kwa kidato cha nne na kukemea utoro wa jumla na rejareja huku akiwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii, akihimiza walimu wa kujitolea kupata bima ya afya pamoja na kuwataka viongozi kuwa wa kuchukua maamuzi ili utekelezaji wa miradi usilale.
Katika hatua nyingine Bw. Moses Rusasa kwaniaba ya Mgodi wa GGML amefurahishwa na hatua za mradi wa Shule ya Sekondari Mkalanga pamoja na miradi mingine, lakini pia ameishukuru serikali na wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kufanikisha utelelezaji wa miradi mbalimbali chini ya fedha za CSR kisha kuahidi kuyafanyia kazi mapungufu ya baadhi ya vifaa kwa baadhi ya maeneo akikiri kuwa hali hiyo hutokea kulingana na uwingi wa maeneo wanayoyasambazia vifaa hivyo vya ujenzi.
Kazi bado inaendelea, endelea kufuatilia ili kupata taarifa zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa