Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela amepokea na kuukaribisha Ujumbe wa Wataalam kutoka Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi, na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini Ghana (GHEITI) ukiwa na wawakilishi 12 wakiwakilisha makundi mbalimbali kwenye Taasisi hiyo kutoka nchini Ghana.
Ujumbe huo umepokelewa Desemba 7, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita, ikiwa ni mara yao ya kwanza, kisha kukutana na Mkuu wa Mkoa Mhe.Martine Shigela na baadaye kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Tume ya Madini, Soko la dhahabu, pamoja na kutembelea kata ya Lwamgasa yenye shughuli za uchimbaji kwa lengo la kujifunza.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa kujifunza, kubadilishana na kupata uzoefu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa kwenye sekta ya uchimbaji nchini Tanzania.
Aidha, ziara hiyo inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja ugeni huo kutoka nchini Ghana, ambapo umekuwepo nchini Tanzania kwa muda wa wiki moja kuelekea kuhitimisha ziara yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa