Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Geita kwa kauli moja imetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Utendaji uliotukuka wa kuliletea Taifa maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati iliyolenga kusogeza huduma za jamii kwa wananchi.
Halmashauri kuu ya CCM imetoa tamko hilo leo januari 19, 2022 kwenye Ukumbi wa Nyerere-EPZA Mjini Geita wakati kamati hiyo ilipoketi mahsusi kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2021 kwa Mkoa huo.
Tamko hilo limekuja baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Mhe. Said Kalidushi kufafanua kuwa Mhe. Rais ameleta fedha nyingi kwenye Miradi mbalimbali Mkoani Geita na kuwa Mkoa wa tatu kwa kupata pesa nyingi zaidi nchini ambapo ndani ya kipindi cha serikali ya awamu ya sita kwenye miradi ya sekta mbalimbali, Mhe. Rais ameleta zaidi ya Tshs. Bilioni 58
"Kazi tumeiona, tumeona jinsi mlivyosimamia fedha za UVIKO na madarasa yanameremeta, sasa tunaomba shughuli zinazofanywa kwa nguvu za wananchi nazo mkazisimamie kama mlivyosimamia pesa hizi." Amesema ndg. Evarist Gervas MNEC Mkoa.
Kamisaa wa CCM Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Kamati yake kwa ufuatiliaji wa kina wa matumizi ya fedha za miradi na Wakuu wa Wilaya ambao wamesimamia kwa karibu miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora.
"Kwa kipindi cha kuanzia januari hadi desemba 2021 tumepokea zaidi ya Bilioni 58 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ukiachia mbali ile miradi ya kimkakati, fedha hizi ni nyingi sana na zimeletwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, TASAF, Nishati ya Umeme na Barabaraba." Amesema
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa