Na Boazi Mazigo- Geita RS
Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Geita kimeendelea kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa vitendo kwa kupita kukagua na kufuatilia utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo kikihimiza ubora na thamani ya miradi.
Hayo yamedhihirika Agosti 23, 2023 wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Geita walipotembelea na kuwatia joto la mafanikio wanafunzi wapya wa kidato cha tano wa shule ya sekondari Mbogwe ambapo wajumbe hao walitumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi hao kutumia nafasi walioipata ili kuzifikia ndoto zao.
Akiongea na wanafunzi hao, mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema "unayesoma ni wewe, shughulika na masomo na yale mapungufu unayoyaona waachie viongozi wayashughulikie. Kwa kuwa mmepata bahati ya kupata Miundombinu mizuri, someni na tutapenda kuna wote mnafauru"
Vilevile Mwenyekiti Kasendamila alisisitiza juu ya wahandisi kuendelea kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi ili kudumisha ubora na tija kwa ustawi wa nchi hii ikiwa pia ni kumuunga mkono kwa vitendo Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia usimamizi ulio mzuri wa miradi
Nao wajumbe wengine kwa wakati tofauti, waliwapongeza wanafunzi hao kwa kufaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo, wakiwataka kuongeza juhudi na kutilia mkazo suala la elimu ili wawe viongozi wa taifa hapo baadaye.
Kwa upande wake Mhe.Cornel Magembe ambaye ni mkuu wa wilaya Geita kwaniaba ya Mkuu wa mkoa geita alisema, "kwaniaba ya serikali mkoani hapa, nawakaribisha sana, na serikali inaendelea kuboresha Miundombinu mbalimbali kupitia fedha zinazoendelea kuletwa na Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Nao bw.Seth Bwire na bi.Felister Vicent ambao ni wanafunzi wa kidato cha tano walitumia fursa hiyo kukishukuru Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na viongozi wa serikali walioambatana nao na kuwaahidi kusoma kwa bidii na kwamba watakapomaliza elimu yao wanaamini watafaulu kwa kishindo.
Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi ya Shs.1,690,657,756.06 ya sekta ya elimu na afya na kuhimiza wahandisi kusimamia miradi kwa ukaribu
Ziara ya kamati hiyo inaendelea mkoani Geita, kituo kinachofuata ni Chato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa