• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Majaliwa Atoa MieziMitatu kwa Wakuu wa Mikoa Kukamilisha Masoko ya Madini.

Posted on: March 24th, 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa hususan mikoa yenye utajiri mwingi wa madini ya metali na vito nchini kuhakikisha wanakamilisha na kufungua masoko ya madini ili kuwawezesha wachimbaji na wafanyabiashara ya madini kuwa na soko la uhakika la madini hayo.

Majaliwa alitoa  agizo hilo kwenye uzinduzi wa Soko la Madini la Geita tarehe 17 Machi, 2019 uliofanyika katika viwanja vya Soko Kuu mkoani Geita na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa kiserikali ikiwa ni pamoja na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.

Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula, watendaji kutoka Tume ya Madini, Wakuu wa Mikoa, wabunge, madiwani, viongozi wa dini, waandishi wa habari pamoja na wananchi kutoka katika mkoa wa Geita pamoja na mikoa ya  jirani.

Alisema kuwa, uanzishwaji wa masoko ya madini ni  sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa tarehe 22 Januari, 2019 kwenye mkutano wake na wachimbaji wa madini nchini uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

“Ninawataka wakuu wa mikoa kuhakikisha agizo hili linatekelezwa kabla ya mwaka wa fedha kumalizika Juni 30, 2019,” alisema Majaliwa.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwanufaisha watanzania wote, Serikali kupitia Wizara ya Madini ilianza kwa kuboresha Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Aliongeza kuwa, serikali imeamua kuondoa tozo mbalimbali zilizokuwa mzigo kwa wachimbaji wa madini uli uchimbaji wao uwe na faida kubwa na kuwawezesha kulipa kodi mbalimbali za Serikali.

Alisema kuwa, kufutwa kwa kodi na tozo mbalimbali kutapunguza kwa kiwango kikubwa utoroshwaji wa madini nje ya nchi na Serikali kujipatia pato kubwa linalotokana na shughuli za madini nchini.

Akielezea umuhimu wa masoko ya madini, Majaliwa alieleza kuwa mbali na kupunguza utoroshwaji wa madini, hakutakuwepo na dhuluma kwa wachimbaji wadogo wa madini kwani watakuwa na sehemu yenye uhakika ya kuuzia madini hayo kulingana na bei elekezi iliyotolewa na Serikali.

Aliendelea kueleza kuwa, soko la madini  litarahisisha huduma za uuzaji na ununuzi wa madini ambapo huduma zote zitatolewa ndani ya jengo moja hivyo kuokoa muda wa wauzaji na wanunuzi wa madini.

Katika hatua nyingine, Majaliwa alitoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa, atakayekamatwa anatorosha madini atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha.

Pia aliwataka viongozi na watendaji wa Serikali kusimamia kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali  kuhusu sekta ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje ya nchi.

Aidha, aliitaka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine za Serikali  zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini kuheshimu mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

“Wizara ya Madini, ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahususi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko hilo ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini,” alisisitiza Majaliwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya  sekta ya madini ambapo utekelezaji  wa dhamira hiyo unakwenda sambamba na kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa sekta ya madini nchini.



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa