MAMA JANETH MAGUFULI ATOA ZAWADI KWA WAZEE 400 WILAYANI CHATO
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amezungumza na kutoa zawadi ya tani 24000 za mchele na unga pamoja na mafuta ya kupikia kwa wazee 400 kutoka katika vijiji tofauti Wilaya ya Chato.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita na wilaya ya Chato mama Janeth ameitaka jamii kuwa na moyo wa kuwasaidia wazee walio katika maeneo mbalimbali kwa kuwa wengi wao hawajiwezi. Amesema kitendo cha kuwasaidia wazee wasiojiweza ni baraka kutoka kwa mwenyezi mungu kwa kuwa wazee wezee wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali pamoja na kukosa chakula.
Katika Hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Dkt. Medard Kalemani Naibu Waziri wa Nishati na Madini kila mzee alipata msaada wa kilo 25 za mchele na unga pamoja na mafuta ya kupikia. Katika hatua nyingine Serikali imesema inatambua mchango wa wazee hivyo itaendelea kuwahudumia na tayari katika Wilaya ya Chato kuna dirisha la wazee katika Hospitali ya Wilaya. Wilaya ya Chato ina wazee zaidi ya 18000 elfu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa