Septemba 27, 2020 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki afunga Rasmi maonesho ya tatu ya Madini Mkoani Geita.
Akifunga maonesho hayo, Waziri Kairuki amewapongeza Wachimbaji wadogo kwa kulipa kodi zinazohusiana na Madini kwa hiari na kufuata taratibu na sheria za Madini Nchini.
Aidha, Waziri kairuki amesema kwa uungwana nuzalendo mkubwa wa wachimbaji kwa Serikali wameifanya sekta ya madini kuchangia pato la Taifa kwa asilimia 5.2 kwa sasa tofauti na asilimia 3.4 za mwaka 2015.
Akitoa salamu za Wizara ya Madini Mhe. Doto Biteko (MB), Wazri wa Madini amesema Serikali imeendelea kutekeleza mipango ya kuwawezesha wachimbaji waweze kufanya shughuli zao kwa Uhuru ili ziweze kuwaletea tija.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita alifafanua kuwa asili ya maonesho ya tatu ya madini 2020 ni mwaka 2018 baada ya kuanza kwa maonesho ya madini ya kwanza yaliyochochewa na mabadiliko ya sheria ya madini mwaka 2017.
Awali, Mhe. David Azaria kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kazi kubwa ya kuuletea maendeleo Mkoa wa Geita huku akisema ameonesha kuwa nia ya dhati ya kutekeleza yaliyomo kwenye ilani ya Chama hicho ya mwaka 2015/20
“Hongereni sana Mabenki na Taasisi zinginge za Fedha kwa kutoa mikopo kwa wachimbaji wa madini kwani hiyo ni hatua kubwa sana kwenye sekta ya madini”. Amesema Mhe. Stansilaus Nyongo Naibu Waziri wa Madini.
Mhe. Costantine Kanyasu Naibu waziri wa Maliasili na Utalii ametoa pongezi kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kwa kufuata matakwa ya sheria ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii ya mwaka 2017 ambapo sasa Mji wa Geita unakua kwa kasi kwa utekelezaji wa Miradi chini ya Mpango huo.
Naye, Mjumbe wa Kamati ya Madini wa muda mrefu na Mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi jimbo la Geita Vijijini Mhe. Joseph Kasheku Musukuma amewataka wizara ya Madini kuendelea kuweka mazingir rafiki kjwa wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwaondolea tozo zinazojirudia.
Wakitoa salamu za Mikoa yao kwenye Hafla hiyo wakuu wa Mikoa ya Tabora na Mara wamemppongeza sana Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa ubunifu mkubwa unaopelekea kuipaisha Geita kimaendeleo.
“tunaipongeza sana Serikali kwa kuifanya Sekta hiikukua kwa kasi na kuifanya kuwa na Mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi.” Amesema Rais wa Wachimbaji wa Madini nhini Ndugu John Bina.
Akitambulisha Wageni Ndugu. Denis Bandisa alifafanua kuwa maonesho ya madini ya mwaka 2020yamewakutanisha wajasiriamali, wachimbaji na makampuni mbalimbali waliokuja kuonesha Teknolojia rahisi za uchimbaji nauchenjuaji wa madini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa