Na Boazi Mazigo-Geita
Katika kuhitimisha maadhimisho miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wananchi wa Geita wameshuhudia ufunguzi wa bweni la wasichana la Shule ya Sekondari Nyakagwe lililopo Kijiji cha Nyakagwe, kata ya Butobela, halmashauri ya wilaya Geita lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 80.
Akiongea na wananchi baada ya kuongoza zoezi la upandaji miti na ufunguzi wa bweni hilo Aprili 28, 2023, mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela alisema, “ujenzi wa bweni hili ni kielelezo cha uongozi na misingi iliojengeka katika misingi ya utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".
"kaulimbiu ya umoja na mshikamano, ndiyo msingi wa kukuza uchumi wetu, hivyo niwapongeze wananyakagwe kwa kubuni mradi wa sekondari, hongereni pia kwa kujali na kuthamini elimu. Wakati wa Korona kupitia ushawishi wa kiongozi wetu mhe.Rais.Dkt.Samia Suuhu Hassan, tulijenga madarasa 640, mabilioni ya BOOST sasa yanamwagika. Hatuna budi kuuthamini muungano, leo tunaadhimisha miaka 59 tunajivunia mafanikio katika sekta za elimu, amani, utulivu na mshikamano. Sisi ni ndugu, jamii moja hivyo tuudumishe".Allisema RC Shigela
vilevile, Mhe.Shigela aliekeza kuwa, kwakuwa bweni hilo limefunguliwa ni vyema litumike mapema muhula ujao na kupitia CSR na vyanzo vingine Halmashauri iweke umeme. Alitumia nafasi hiyo kukemea waganga wakuu wilaya ikiwa watahusika na uhujumu wa dawa kwenye hospitali na kutoa wito kwa jamii kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na kuwalinda wanawake na wajane dhidi ya manyanyaso.
Mwisho alisisitiza umuhimu wa kujiunga na bima iliyoboreshwa akiwataka wamiliki wa migodi kuwakatia bima wafanyakazi wake, kisha kutoa tuzo kwa wanafunzi walioshinda mashindano ya insha ya muungano na kuchangia Laki 5 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya michezo kwa shule hiyo.
kwa upande mwingine, katibu tawala mkoa Geita Prof.Godius Kahyarara alisema, "kama mkoa tumeendelea kutekeleza maagizo ya viongozi wetu ikiwemo ufunguzi wa mradi huu uliochaguliwa kitaifa. Vilevile nipongeze wasimamizi wa mradi huu, thamani ya mradi inaonekana, na wetu sisi huu ni mfano wa kuigwa, hivyo tuudumishe muungano".
Naye mkuu wa wilaya Geita Mhe.Cornel Magembe alisema, " awali ma DC tulipata changamoto ya kutafuta namna ya kujenga miradi hii, lakini kwa sasa Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan anatafuta na kutuletea, tumuunge mkono, kazi yetu ni imekua nyepesi, ni kuzisimamia. Nikemee pia wale wote wanaowamendea wanafunzi wa kike, hawa ni watoto wa serikali. Niseme tu kuwa, kama wilaya tunashukuru serikali kwakuwa tangu mwaka wa fedha uanze hadi hivi leo, wilaya ya Geita tumepokea bilioni 11 kw ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa".
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande alisema " nilizoea kuona fedha za TASAF zikigagiwa kaya masikini pekee, lakini sasa zinajenga miradi, asante Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan na hakika Geita unatutendea mema"
Diwani wa kata ya Butobela na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Geita Mhe.Charles Kazungu aliishukuru serikali akisema uwepo wa shule hiyo umepunguza umbali Km 7 hadi 8 kwa wanafunzi hivyo kutoa ombi kwa serikali kuendelea kusogeza karibu miundombinu ya maji na umeme.
Akisoma taarifa ya mradi huo, mtendaji wa kata ya Butobela Reuben Makala alisema ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi 80 wa kike wa shule ya sekondari Nyakagwe umegharimu zaidi ya Milioni 157 ambapo kati ya hizo, 10% ni nguvu za wananchi na kiasi kingine ni fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF TPRP/OPEC IV ambapo kama wananchi wanatoa shukrani za dhati kwa serikali inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo wanaamini mradi huo utaondoa changamoto ya mimba za utotoni na kupunguza umbali mrefu na kuchochea ufaulu.
“Miaka 59 ya Muungano, Umoja na Mshikamano Ndiyo Nguzo ya Kukuza Uchumi”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa