Na Boaz Mazigo- Geita RS
Halmashauri mkoani Geita zimetakiwa kuhakikisha zinakamilisha miradi ya maendeleo kwa kuzingatia ubora na wakati ili wananchi wasikose fursa ya kuitumia na kupitia miradi hiyo waweze kujiletea maendeleo.
Wito huo umetolewa katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Novemba 22, 2023 na katibu tawala mkoa wa Geita Bw. Mohamed Gombati wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na watumishi wa umma hukupamoja na mengine akisisitiza uwajibikaji, ushirikishwaji wananchi kwenye utekelezaji wa miradi , ushirikiano baina ya watumishi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati na baada ya kutembelea miradi mitatu ua sekta ya elimu na afya yenye thamani za zaidi ya Bilioni 1.2, bw. Gombati alisema lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuona Mwananchi ananufaika kiuchumi na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali, hivyo ni muhimu kuikamilisha kwa wakati.
“kwanza niwapongeze wanambogwe kwa utekelezaji wa miradi, lakini pia ieleweke yakuwa, lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na iwanufaishe wananchi, hivyo ni vyema kukamilisha miradi kwa wakati lakini kwa usimamizi ulio madhubuti”, alisema bw. Gombati.
Aliongeza kuwa, ni vyema viongozi kukemea uzembe kazini na wale wanaobainika kufanya ubadhirifu wachukuliwe hatua, lakini pia taasisi zinazotoa huduma kama TANESCO zihakikishe huduma hizo zinafika kwenye shule zinazojengwa.
Mwisho, Bw.Gombati alisisitiza juu ya mamlaka za serikali za Mitaa kuhakikisha taasisi za serikali kama shule na miundombinu mingine inapimwa na inapatiwa hati za umiliki kwani huo ni utelezaji wa matakwa ya sheria lakini pia hupunguza migogoro.
Kwaniaba ya wananchi wa Mbogwe, mkuu wa wilaya hiyo mhe.Sakina Mohamed alisema, maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi huyo yatazingatiwa na hivyo kazi itaendelea kwa kasi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa