• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa Geita awataka wananchi Kujitokeza kwa Wingi kwenye Elimu kwa Mlipa kodi

Posted on: April 9th, 2018

Mkuu wa Mkoa Geita awataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni ya Elimu kwa Mlipa Kodi  

Wito umetolewa kwa wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi katika Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko, changamoto, maoni pamoja na kupata elimu ya masuala ya kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Geita, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa, wafanyabishara na wananchi watumie fursa ya kampeni hii itakayomalizika tarehe 13 Aprili, 2018 kupata elimu sahihi ya masuala ya kodi na tozo mbalimbali.

"Nachukua fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi wote wa mkoa huu hususani wale wanaoishi katika maeneo ya Masumbwe, Ushirombo, Rulembela, Katoro, Lunzewe, Namonge, Nyanghw'ale, Bwanga na Muganza kujitokeza kwa wingi ili waweze kujifunza, kupata huduma na kutoa maoni yao kwa watalaam wetu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kuyatolea ufafanuzi na kuyafanyia kazi," amesema Mhe. Luhumbi.

Nae Meneja wa TRA mkoani hapa, James Jilala amesema kuwa, lengo kuu la kufanya kampeni hii maalumu ni kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea mrejesho na maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

"Kampeni hii ni mwendelezo wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika nchi nzima kuanzia tarehe 5 hadi 9 Machi, 2018 katika ngazi ya mkoa. Kutokana na matokeo ya kampeni ile mkoani hapa, tumeona ni muhimu tuwe na kampeni nyingine maalumu ambayo inafanyika maeneo mbalimbali katika wilaya zetu tofauti na ile ya kwanza iliyofanyika Geita mjini tu," amefafanua Jilala.

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya watalaam kutoka TRA Makao Makuu Maternus Mallya ameeleza kuwa, timu yake imejipanga vizuri na tayari kazi imeanza kufanyika katika vituo vyote vilivyotengwa kwa ajili ya kampeni hiyo.

"Hapa ninapozungumza, wenzangu wako kwenye maeneo husika wanaendelea kufanya kazi. Hivyo, kama alivyosema Mhe. Mkuu wa Mkoa, nami natoa rai kwa wananchi wote mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi ili waweze kukutana na watalaam wetu kwa ajili ya kupata huduma na elimu ya mlipakodi," amesema Mallya.

Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani Geita imeanza leo tarehe 9 hadi 13 Aprili, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyabiashara na wananchi watasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kuelimishwa kuhusu ulipaji wa Kodi ya Majengo kwa njia ya kieletroniki.

Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa