• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mwananchi Kuwa Chachu ya Maendeleo ya Taifa Lako- DC Komba

Posted on: December 10th, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Hashim Komba amewaasa wananchi wa Wilaya ya Geita kushiriki kuinua uchumi wa Nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa wazalendo sambamba na kutafakari kwa kina ndani ya miaka 63 ya Uhuru wa Nchi ya Tanzania walipotoka, walipo sasa na wanapoelekea .

Mhe. Komba ameyazungumza hayo alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela kwenye Kongamano la Wadau lililofanyika katika Ukumbi wa Gedeco Halmashauri ya Mji wa Geita wakati wa Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Geita ameeleza kuwa waasisi wa Nchi ya Tanzania walitumia uwezo wao na uzalendo wa hali ya juu kuifikisha Nchi   mahali ilipo hususan mafanikio katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, maji, barabara na nyinginezo.

Akizungumza namna maisha yalivyokuwa kipindi Nchi ya Tanzania inapata uhuru, Mzee Samwel Majura ambaye ana umri wa miaka 75 ametoa rai kwa vijana wa sasa kuacha tabia ya kuibeza Serikali kuwa haijafanya lolote wakati katika kipindi cha nyuma wananchi walitembea umbali wa Zaidi ya kilomita 20 kufuata huduma za afya katika Hospitali moja tu iliyokuwa Geita mjini hali iliyopelekea baadhi ya kina mama kujifungulia njiani, lakini ndani ya miaka 63 ya Uhuru Serikali imejenga zahanati kila kijiji na vituo vya afya vya kutosha.


Kwa upande wake Mzee James Zomola mwenyeji wa Wilaya ya Geita ambaye alianza elimu yake katika darasa maarufu kipindi hicho “Bush School” ameeleza kuwa wakati Nchi inapata uhuru kutoka kwa wakoloni shule zilikuwa chache sana na hakukuwa na walimu wa kutosha hali iliyosababisha wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo, kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari ilikuwa ni bahati sana lakini sasa hivi Serikali imejenga shule nzuri za sekondari kila kata zikiwa na walimu wa kutosha.

“ Mimi binafsi naweza kutoa ushuhuda wa Sekta ya maji kwa namna ambavyo ndani ya kipindi cha miaka 63 ya Uhuru imeboreshwa kwa kiwango kikubwa sana, wananchi wanapata huduma za maji majumbani kwao au jirani kabisa na maeneo wanayoishi tofauti na miaka ya nyuma ambapo maji yaliyotumika yalitokana na chemichemi, mito na maziwa. Nakumbuka kwa wakazi wa Kata ya Kasamwa ambao chanzo chetu cha maji ilikuwa ni chemichemi wakati wa kiangazi maji yalikuwa yanakauka na kulazimu watu wenye baiskeli tu kufuata maji Geita mjini katika kisima cha asili Lwenge.” Aliongeza Mzee James Zomola.

Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara   yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara: Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu.”  wananchi wa Wilaya ya Geita waliohudhuria katika Kongamano la Uhuru walipata kufahamu Historia ya harakati za kupata Uhuru wa Tanzania na mchango wa viongozi wa Taifa katika Maendeleo ya kiuchumi, Tanzania na harakati za mapinduzi ya kiuchumi katika sekta za elimu, afya, maendeleo ya jamii, kilimo, miundombinu, nishati, biashara, mawasiliano na ujenzi kupitia mada zilizowasilishwa na wataalam wa kada mbalimbali.



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Waziri Mavunde Aaagiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nyuma Ya CSR Geita

    April 15, 2025
  • Mabonanza ya Watumishi Yawe Endelevu - DC Kingalame

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa