• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mwenye Macho Aambiwi Tazama, Daraja la JP Magufuli 76.34%

Posted on: September 9th, 2023

Na Boazi Mazigo - Geita RS

Katika hali ya furaha na moyo uliojawa tabasamu, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita wamefarijika na hatua ya maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa Km.3 na barabara unganishi zenye urefu wa Km.1.66 kwa gharama ya shilingi bilioni 716.3 ambapo wameonesha kuridhishwa na hatua ya mradi huo kisha kumpongeza Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan na kumuombea dua na afya njema ili aendelee kuwatumikia watanzania.

Hayo yamejiri Septemba 8, 2023 wakati wajumbe halo walipozulu kwenye eneo linapojengwa daraja hilo (kigongo-busisi) na kutoa wito kwa wakazi wa Geita kujiandaa kutumia fursa ya uwepo wa daraja hilo lakini pia kuwasihi wataalam watanzania wanaosimamia ujenzi huo, kuhakikisha linakuwa na kiwango na ubora uliokusudiwa.

Akiongea kwa nyakati tofauti, mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema, "hakika mwenye macho aambiwi tazama. Tumshukuru na kumpongesa sana Rais wetu mpendwa, tumuombee kwa Mungu aendelee kuwa na hekima na busara na viongozi twende tukaisemee miradi hii wananchi waijue na kama CCM tunaunga mkono juhudi hizi kwa 100%".

Mwenyekiti Kasendamila aliongeza kuwa wajumbe hao walifika hapo kwa lengo la kuona, kujifunza na kisha kwenda kuisemea miradi ikiwemo wa daraja hilo kisha kumpongeza mhe.Martine Shigela, mkuu wa mkoa Geita kwa namna alivyo na ushirikiano, msikivu na mshauri kwenye chama.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Geita Mhe.Martine Shigela alisema, ‘serikali imetekeleza, daraja hili ni mkombozi kwa maendeleo ya wananchi wetu. Tumshukuru sana mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwakuwa alipoingia madarakani, daraja hili lilikuwa kwenye 25% ya utekelezaji lakini hadi sasa lipo 76.34% kama tulivyoelezwa na mtaalam. Ajira nyingi zimepatikana kwa wazawa na wananchi anzeni maandalizi kutumia daraja hili kiuchumi".

Awali akitoa maelezo ya mradi, mhandisi William Sanga ambaye ni msimamizi wa mradi kutoka wakala wa barabara nchini TANROADS Mwanza alisema, mradi huo unafadhiliwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na muda wa utekelezaji ni miezi 48 kuanzia tarehe 25 februari, 2023 na hivyo unarajiwa kukamilika ifikapo februari 24, 2023 wenye gharama ya bilioni 716.3 na utakapokamilika utaondoa uwezekano wa kutokea vifo vinavyoweza kutokea kutokana na ajali za vyombo vya kuvukia eneo hilo. Vilevile alisema, muda wa kuvuka utakuwa ni dakika 4 kutoka zaidi ya Saa mbili za kupitia kwenye feri kwa sasa.

Mhandisi Sanga aliongeza kuwa, mradi huo mpaka sasa umetoa ajira 1,001 ambapo kati ya hizo, 944 zimetolewa kwa watanzania na 57 kwa raia wa kigeni na kwamba daraja hilo litakapokamilika litakuwa daraja la sita (6) katika Bara la Afrika likitanguliwa na madaraja ya 6th October Bridge (Misri) mita 20,500, Third Mainland Bridge (Nigeria) mita 11,800, Suez Canal Bridge (Misri) mita 3,900, Mozambique Island Bridge (Msumbiji) mita 3,800 na Dona Ana Bridge (Msumbiji) mita 3,670.

Ziara hiyo ilihitimishwa baada ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mkoa Geita kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita, uwanja wa ndege Geita (Chato), stendi ya mabasi Kahumo, Bandari ya Nyamirembe, hospitali ya rufaa ya kanda chato pamoja na kuzulu katika kabuli la Hayati Dkt.John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.









Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa