Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Inmi Patterson ametembelea na kufanya kikao na viongozi wa Mkoa wa Gieta wakiwemo wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
Kaimu Balozi Dkt.Patterson ameshukuru kwa mapokezi kutoka Geita huku akieleza nia ya ziara yake akizungumzia hasa masuala ya Elimu na Afya na kuonesha haja kuongeza kasi ya mapambano ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi kufikia asilimia sifuri (0) lakini pia kupata uzoefu zaidi juu ya eneo la madini kwakuwa Geita inafahamika kutokana na uwepo wa madini, hasa dhahabu.
Amesema, nimetembea kwa usafiri wa gari hadi Geita lengo nijifunze na kuangalia maisha ya mtanzania kwa uhalisia. Ningependa kuona asilimia ya maambukizi ya VVU yanafikia asilimia sifuri (0) kwakuwa tumekua tukishirikiana kutokomeza ugonjwa huu. Tunapenda vilevile kujua maendelea katika sekta ya elimu na afya kwani mwalimu alisema, maendeleo ya ukweli ni maendeleo ya watu”
Dkt.Patterson amesisitiza juu ya utoaji endelevu wa elimu na hamasa kwa wananchi ili waendelee kujitokeza kupima na endapo wamegundulika wana maambukizi basi waanze matumizi ya ARV mara moja na ikiwezekana zipatikane za miezi sita (6) kwa awamu moja.
Akiongea wakati wa kuukaribisha ugeni huo, Mhe.Eng Mtemi Msafiri kwaniba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, ameeleza kufurahishwa na ujio wa mwakilishi huyo wa taifa kubwa duniani huku akisema, “ tunashukuru kwa namna Marekani ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa nchi yetu, lakini pia tunafurahia ujio wenu hii ni bahati kwetu kwakuwa tunajua yakuwa mgeni njoo mwenyeji apone” na kuomba ubalozi huo kwenda na wazo la kuboresha kilimo cha umwagiliaji kwa wakazi wakaao pembezoni mwa Ziwa Viktoria, ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza umasikini, lakini vilevile kupunguza kasi ya maambukizi kwa kutoa ajira kwa vijana kwa kuwatengenezea miradi ya uzalishaji.
Mhe.Eng. Msafiri amemhakikishia Dkt. Patterson juu ya uwepo wa utashi wa viongozi wa kisiasa katika mapambano dhidi maambukizi ya VVU na kuomba nchi hiyo iendelee kuunga mkono jitihada zinazofanywa nchini hasa sekta ya elimu kutokana na mwitikio wa wanafunzi kuongezeka kutokana na elimu bila malipo.
Kuhusu maeneo ya wachimbaji wa madini, Mhe. Eng. Msafiri ameomba msaada kwenye eneo la teknolojia bora ya uchimbaji wa madini ya dhahabu kwakuwa kuna uharibifu mkubwa unaotokana na matumizi ya miti alimaarufu kama Matimba kwenye mashimo ya dhahabu, kisha kumuahidi kujitahidi kuendelea kutoa elimu ili kupunguza maambukizi ya VVU na kuhamasisha jamii kupima na kujikinga, kisha ugeni huo kuendelea na ziara yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa