Jumla ya nyumba 20 za makazi za askari polisi zimefunguliwa kwaniaba ya nyumba 114 zilizokamilika nchi nzima kati ya nyumba 400 zilizopo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji, tukio lililofanyika julai 15, 2019 katika Mtaa wa magogo kata ya bombambili, Mjini geita.
Akifungua nyumba hizo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Jeshi la Polisi nchini kwa jinsi wanavyotekeleza mradi huo vizuri huku wakitumia nguvu kazi “force account”, jambo lililowawezesha kuanza ujenzi wa nyumba 400 kwa Bil 10 alizozitoa wakati wa kumbumbuku ya Hayati Abeid Amani Karume Mwezi Aprili mwaka 2108 Mkoani Arusha, huku akitangaza uamuzi wa kutoa milioni 1,500 kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya katoro (halmashauri ya wilaya ya geita) akisema si vibaya kuwa na hospitali mbili za wilaya kwenye wilaya moja.
Rais Magufuli amesema, “niwapongeze Wizara na Jeshi la Polisi kwa ujenzi wa nyumba hizi, niwapongeze wadau wetu mbalimbali kwa kuunga jitihada za serikali za uboreshaji makazi ya askari polisi, kwa kujenga Nyumba 49 nchi nzima. Nina imani kuwa nyumba hizi zitasaidia kuboresha utendaji wa askari wetu. Nawapongeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa mnaoyifanya kuhakikisha nchi na mipaka yake inakuwa tulivu na amani”.
Rais Magufuli ameendelea kusema kuwa, serikali inatambua changamoto za makazi ya askari bado ni kubwa, hivyo kuwahakikishia kuwa, kwa kadiri uwezo wa serikali utakavyokua na kuimarika, suala la nyumba litaendelea kushughulikiwa pamoja na changamoto nyingine. Pia ametoa wito kwa askari wa jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo.
Katika hatua nyingine, Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro amepongezwa na Rais Magufuli kwa hatua za kinidhamu anazozichukuwa kwa askari polisi wachache wasio waadilifu, kwani kuanzia Januari hadi juni 2019, jumla ya askari 157 wamechukuliwa hatua wakiwemo Maaskari wanaobambikizia raia kesi, wanaohusika na ujambazi pamoja na kuonea raia, ambapo askari 54 wamefukuzwa kazi.
Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujipanga na uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye mwakani uchaguzi mkuu na kuwaasa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuchapa kazi kuinua uchumi wao. Wakati huo huo, mbunge wa jimbo la geita Joseph Kasheku Msukuma kuelezwa kuwa, ni vyema kuandaa nyumba za askari katika jimbo lake ili askari alioomba wapelekwe mara moja.
Jeshi la polisi limeagizwa kuhakikisha nyumba 286 zilizobakia zinakamilika haraka na watakaopewa nyumba hizo vilevile wametakiwa kuzitunza, na pia kambi ya hiyo ya polisi kupewa jina la IGP Sirro kisha Rais Magufuli kusema, “wafanyabiashara wa madini tumieni masoko yaliyowekwa na serikali, itatusaidia kujua kiasi cha dhahabu inayozalishwa, uchumi utainuka”.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Luloga ametoa shukran kwa Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi na kwamba ulinzi na usalama uliyopo nchini ndiyo unawafanya wageni waje Tanzania Kuhiji, lakini uwezeshaji wa fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba hizo ni uwekezaji katika jeshi hilo na ni kuthamini mchango wao, hivyo hawatamuangusha, kisha kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na kamati ya Usalama Mkoa kwa kazi nzuri mkoani geita.
Waziri Lugola amesisitiza kuwa, anaamini nchi imepata kiongozi sahihi, mpole na mchapakazi hivyo ataendelea kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika kwani bila hivyo wakati wa uchaguzi ni vigumu kupata viongozi wazuri kama hakuna amani.
Akisoma taarifa ya mradi, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro ametoa pongezi za shukrani kwa Rais Magufuli kukubali kuwa mgeni rasmi na pia kwa jinsi ambavyo analijali jeshi la polisi akitoa mifano kadhaa ikiwemo kupewa Bil 10 kwaajili ya makazi ya askari polisi, kupewa Bil 3.5 kwaajili ya ununuzi wa Helikopta, kupewa Mil 700 za ukarabati wa chuo cha kilwa road huku akisistiza nidhamu kwa watumishi wa jeshi la polisi.
IGP Sirro ametaja takwimu za upungufu wa idadi ya matukio akianza na ya uhalifu kuanzia mwezi januari–Juni 2018 na Januari – Juni 2019 kuna upungufu mkubwa kama ifuatavyo; uhalifu wa jumla, upungufu ni 2.2%, makosa makubwa ya usalama barabarani, upungufu wa matukio 610, sawa 27.5 %. Kwa upande wa matukio yanayosababisha vifo, kuna upungufu wa matukio 175, sawa 22.3%. Matukio ya misiba (watu waliofariki) upungufu wa ajali zinazosababisha vifo ni 25.7% na waliojeruhiwa, upungufu ni takribani 30.8%, hivyo upungufu ni mkubwa ukilinganisha na mwaka jana.
IGP Sirro amemaliza kwa kusema, nyumba hizo zimejengwa kila mkoa kwa gharama ya Tshs. Mil 25 kwa Nyumba moja ya vyumba 2 vya kulala, sebule,Jiko, Bafu na choo pamoja na baraza 2 na kwamba nyumba hizi si za maafisa wenye vyeo kuanzia wenye nyota moja. Vilevile IGP Sirro amemuahidi Rais Magufili kuwa, nyumba zilizobaki zitakamilika kufikia mwezi julai 30, 2019 nyumba zote zitakamilika, kisha kuwashukuru kamati ya usalama mkoa wa geita pamoja na wadau waliojenga nyumba 18.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa