RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU AZINDUA NYUMBA 50 ZA WATUMISHI MIKOA YA GEITA, KAGERA NA SIMIYU
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini W.Mkapa amezindua mradi wa nyumba 50 za watumishi wa Idara ya afya katika mikoa ya Geita,Kagera na Simiyu ambazo zimetekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali, Global Fund pamoja na Taasisi ya Benjamini Mkapa Foundation kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5
Awali akizungumza katika kijiji cha Mkungo Wilayani Chato ambapo uzinduzi umefanyika Mheshimiwa Mkapa amewataka wananchi kutunza na kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa ili isaidie wananchi wote.
Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Zahanati ya kijiji cha Mkungo Mheshimiwa Mkapa aliambatana na Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, mama Anna Mkapa na Balozi wa Japani nchini Masaharu Yoshida.Nyumba hizo zipo katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu ambapo Mkoa wa Geita umepata nyumba 20, Kagera 10 na Simiyu nyumba 20.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa