RC Geita Mhe.Rosemary Senyamule Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale Kufuatia Kupata Hati Inayoridhisha Mfululizo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 na 2020/21.
Ameyasema Hayo Leo Juni 21, 2022 Wakati Akiongoza Kikao Maalumu Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Nyang'hwale Huku Akisisitiza Juu ya Mambo Mbalimbali Ikiwemo Halmashauri Kuhakikisha Inapeleka Kodi ya Zuio TRA kwa Wakati.
"Niwapongeze Nyang'hwale kwa Kuendelea Kuwa na Hati Safi, Hii Inaonesha Jitihada Zinazofanyika Katika Kukuza Uchumi wa Nchi Yetu"
Amesema Mhe. Senyamule
Pia Amesema "Ninakemea Uzembe Utokanao na Baadhi ya Watumishi wasiotambua Majukumu Yao ya Utendaji Kazi na Kusababisha Shughuli Nyingine Kukwama Kama Ucheleweshwaji wa Vifaa vya Ujenzi Lakini Pia Kusababisha Hoja kwa Uzembe"
Alisema, ni Muhimu kwa kila Halmashauri Kuendelea Kutunza Mazingira Ukizingatia kwa Nyang'hwale Kuna Uchimbaji wa Madini.
Alisisitiza pia Kupitia Kikao Hicho Akisema, "Naomba Kupata Taarifa za Majibu ya Hoja Kila Nifanyapo Ziara ili Kuweza Kuona Maboresho Katika Utendaji Kazi.
Aliongezea "Madiwani Niwaombe Tuisemee Serikali Wananchi Wajue ni Nini Inafanya Kwani Tukikaa Kimya Wengine Wataisemea Isivyo"
Akimaliza Kabla ya Kuahirishwa Kikao, RC Senyamule Alikumbusha Juu ya Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi na Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kusema Kuwa Ofisi ya Mkoa Itaendelea Kutoa Ushirikiano ili Kuhakikisha Zoezi Hili Linaenda kwa Weledi wa Hali ya Juu.
Awali, Mkaguzi Mkuu wa Nje (M) Geita CPA Richson Ringo Aliwasihi Watumishi na Viongozi Kufanya Kazi kwa Kuzingatia Taratibu, Miongozo na Sheria Mbalimbali Zikiwemo za Bajeti, Fedha, Kazi, Manunuzi n.k ili Kupunguza Uwezekano wa Hoja.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Jamhuri William akasema, "bado nyang'hwale tuna nafasi ya kuongeza mapato ya ndani lakini pia tujitahidi kutimiza wajibu wetu ili kusaidia ukamilishaji wa miradi kwa wakati kwakuwa miradi mingi huchelewa kutoka na baadhi kutotimiza vyema majukumu yao"
Kwa Upande Wake Bi. Sania Mwangakala Ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Alisisitiza Kuwa Halmashauri Zapaswa Kuzingatia Kuwa kwa Sasa Zinapimwa Kupitia Vigezo Vitano Ikiwemo Utekelezaji wa Hoja za CAG, Ukusanyaji wa Mapato, Upelekaji 40% ya Mapato ya Ndani Kwenye Miradi ya Maendeleo, Kutoa Mikopo ya10% ya Mapato ya Ndani kwa Kundi la Vijana, Wanawake na Wenye Ulemavu, Lakini Pia Kufuatilia Marejesho ya Mikopo Hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Bw. John John Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Husna Toni Walisema kwa Nyakati Tofauti Kuwa Wanaishukuru Ofisi ya Mkoa kwa Ushirikiano na Kwamba Wataendelea Kutoa Ushirikiano kwa Wakaguzi Ili Kuondoa Hoja Zilizosalia na Kwamba Watajitahidi Kuongeza Nguvu Kwenye Kuongeza Vyanzo vya Ukusanyaji Mapato.
Boazi Mazigo
AG.HGCU
Juni 21, 2022
Nyang'hwale-Geita
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa