Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameendelea kufurahia matunda ya kuzuiwa kwa Carbon kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine pale alipokuwa akifungua kiwanda cha kuchenjua na kuchakata madini ya dhahabu chenye jina Jema Africa kilichopo mjini Geita eneo la Nyanza mtaa wa Mbugani, eneo lilitotengwa kwa ajili ya shughuli za elution plant terehe 21.07.2018.
katika hotuba yake, Mhe. Mhandisi Gabriel amesema "tunafahamu jitihada za mhe.Rais kuhakikisha rasilimali za nchi hii kubaki salama lakini pia kuwanufaisha wananchi, mabadiliko chanya kwa kuacha mapato stahiki eneo husika lakini pia inaleta maendeleo, hivyo mmiliki wa kiwanda hiki amefanya uamzi sahihi kuja kuwekeza hapa. Amesema pia yeye kama mwakilishi na msaidizi wa Mhe. Rais mkoani Geita, atahakikisha mapinduzi kwa wawekezaji na jamii yanaonekana, vilevile agizo la serikali kupitia Wizara ya Madini la kutosafirisha Carbon limekua na muitiko chanya upande wa viwanda ambapo amefungua Elution Plant hiyo kati ya saba ambazo ni mpya mjini Geita.
Ameendelea kupongeza ubunifu walioufanya Jema Elution Plant kwa kuandaa vyumba vya kupumzikia wateja wakati wakisubiri dhahabu yao. "hii ni njia nzuri ya kumwondolea mteja hofu tofauti iliyokuwepo kabla ya zuio hilo pamoja na kuwa na kamera za ulinzi mambo sasa ni mazuri, na wengine muige kutoka Jema", aliongeza. sambamba na hilo alimweleza mmiliki wa kiwanda hicho kuhakikisha wafanyakazi wake wanapewa mikataba, wanahamasishwa kujiunga na bima ya afya, lakini TRA kuchukua kodi kwenye mishahara kwa mujibu wa sheria, kuzingatia masharti ya usalama kazini na NSSF pia imetakiwa kutembelea Plant hizo ili kuelimisha wafanyakazi juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii bila kusahau wajibu wa kulinda mali ya mwajiri na mteja ili kuzidisha uaminifu kwa mteja. RC Gabriel amesisitiza juu ya usimamizi wa sheria ya madini Na.6 ya mwaka 2010, (3)(a&b) ambapo endapo atabainika anaeendelea kufanya shughuli za madini bila kufuata sheria basi atashughulikiwa. Amemaliza kwa kukagua na kuweka jiwe la ufunguzi wa kiwanda hicho akisisitiza kuwakaribisha wawekezaji wakubwa Mkoani Geita
Mwakilishi wa Ofisi ya Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Bw. Godfrey R. Kelaka ameeleza katika taarifa aliyoisoma kuwa, kwa mwezi juni, 2018 kiasi cha Dhahabu kilichozalishwa baada ya zuio la kusafirisha carbon nje ya Mkoa ilikua kilogramu 104 (kg.104) na kwa mwezi julai 2018 hadi tarehe 19.07.2018 jumla ya kilogramu 97.855 (kg.97.855) na kupata Shilingi Milioni Mia Tano Hamsini (Tshs. 550,000,000/=) kama kodi kutokana na uzalishaji huo na kuongeza kusema kuwa, hali ikiendelea vizuri kufikia mwisho wa mwezi julai 2018 inaweza kupatikana Shilingi Milioni Mia Nane (Tshs. 800,000,000/=) jambo ambalo halikuwahi kutokea kwa wachenjuaji wa aina hiyo.
Mkurugenzi wa Mji Geita, Eng. Modest J. Apolinary ameendelea kuwakumbusha wawekezaji wakaribie Geita kwani eneo lipo zaidi ya Heka 902 kwa uwekezaji wa Elution Plants lakini pia awahaidi ushirikiano wawekezaji Mjini Geita.
Katibu wa CCM Wilaya ya Geita Bw. Julius Peter amesema kama chama wanaamini kasi inayoendelea ya kutekeleza Ilani ya Chama Tawala inatekelezwa kwa vitendo na kwa spidi inayotakiwa kama aliyonayo Mhe. Rais hivyo kuhimiza kutopungua kwa kasi hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Jema Africa Bw. Jumanne Mokili ambaye ni mtanzania aishiye Nchini Japan amesema, changamoto iliyokuwepo kubwa ni ya umeme ambayo imepewa ufumbuzi hivyo kwa changamoto zitakazojitokeza, ofisi yake itaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuzitatua. Kingine ameshukuru kwa serikali kuona thamani ya uwekezaji wao kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa timu nzima kuanzia Halmshauri mpaka Sekretarieti ya Mkoa. Ameahidi pia watahakikisha wanasimamia sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji shughuli zao lakini pia kulinda maslahi ya wafanyakazi na kulipa kodi stahiki kwa serikali..
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa