• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Rc Geita Atembelea Miradi ya Huduma za Jamii, Ahimiza Ukamilishwaji Wake kwa Wakati

Posted on: July 11th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mandisi Robert Gabriel ameendelea kufuatilia hatua za utekelezaji wa Miradi mbalimbali Mkoani Geita kwa kufanya ziara na kuona miradi inayotekelezwa kwa fedha za Huduma kwa Jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).

Ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mzunguko wa Kisasa (Round About) inayojengwa Halmashauri ya Mji wa Geita. Awapongeza mafundi, ashauri ujenzi uendelee siku zote ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.

 Mhe. Mandisi Gabriel amesema na wasimamizi wa mradi kwa kusema, ‘zingatieni thamani ya fedha (Value for Money) na ubora, lakini pia ikibidi mnara unaojengwa ukamilike kabla ya mwaka kuisha kwa kuwa sisi waandisi tukiwa na sikikuu nchi haitajengwa’. Pia amesifu usanifu wa mchoro wa Mnara utakao kaa katikati ya Round About hiyo ukiwa na uwakilishi wa vitu mbalimbali mfano alama ya Mwenge wa Uhuru (uwakilishi wa taifa letu), Matofali ya Dhahabu (alama ya utajiri wa madini) lakini pia itakuwepo saa ambayo inaonyesha kiwango cha joto.

Kwa upande mwingine, Mhe. Mandisi Gabriel ameushukuru uongozji wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji 2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya  Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule. Mkuu wa Mkoa kwa mara nyingine akasema; angependa kuona ujenzi wa Shule hiyo inaanza mara moja, maboma yakamilike ndani ya miezi mwili na nusu, kisha ukamilishaji ufuatie na yeye atashiriki kwa kuwa msimamizi wa shughuli ya ujenzi akizingatia thamani ya fedha hivyo aliwataka wananchi kuanza usafi mara moja kwani tayari baadhi ya vifaa vya ujenzi kwa nguvu za wananchi vipo kwenye eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa alisisitiza kwa kusema, “kwa kuwa tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Tawala CCM, na kwa kasi ninayoiona, tukikaa vizuri kufikia mwakani, Zahanati kila Kijiji tunamaliza kabla ya Uchaguzi Mdogo wa mwaka 2019 kwani maboma yakikamilika tutakuwa juu ya asilimia 80 upande wa Sekta ya Afya. Hata kwa upande wa elimu, maendeleo siyo mabaya” aliongeza.

Alipofika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mhe.Mandisi Gabriel aliona mifuko 680 ya saruji na kupokea taarifa iliyoeleza kuwa bado mifuko 1,459 haijawasilishwa na kwamba kufikia wiki ijayo itakuwa imefika. Lakini pia aliagiza ujenzi uanze wiki inayofuata kwakuwa anapanga kutembelea utekelezaje wake.

Miongoni mwa alioambatana nao katika ziara hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Herman C. Kapufi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita pamoja na wawakilishi wa Mgodi wa Dhahabu Geita GGM



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa