Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewasainisha Mkataba wa Usimamizi wa Lishe Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Geita ikiwa ni utekelezaji wa Maagizo ya Serikali kupitia Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita tarehe 01.10.2018.
Mhandisi Gabriel amesema kuwa, “Geita haijafanya vizuri katika suala la lishe, hivyo Afisa Lishe kwa kushiirikiana na Halmashauri na Wakuu wa Wilaya mnatakiwa kujua vizuri suala hili ili kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii”. Na amesema katika ziara atakzofanya kwenye wilaya hivi karibuni atapenda kusikia maendeleo upande wa lishe.
Pia ametoa wito kwa viongozi kuendelea kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yatokanayo na kutofuata kanuni za lishe ili kutokwama katika kutekeleza majukumu yao, kisha kuwasainisha mkataba Wakuu wa Wilaya.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Denis Bandisa yeye alieleza vipaumbele katika kusimamia suala la lishe ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za lishe, kuandaa mpango mkakati wa lishe wa mkoa, utendaji makini wa kamati ya lishe ya mkoa, usimamizi shirikishi, kutoa vidonge vya kuongeza damu kwa akinamama wajawazito n.k, ya kwamba endapo yatafanyiwa kazi vizuri, basi tatizo la kutokuwa na lishe bora litaondoka. Aliongeza kuwa ,tayari Mkoa umeshaandaa mkakati ili kuanza utekelezaji. Hivyo awaasa viongozi kuzingatia kanuni za lishe na kutokuwa na tabia zisizo nzuri za ulaji kama vile kunywa pombe kupita kiasi.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo imehudhuliwa pia na wakurugenzi na wakuu wa Idara na Vitengo
Mwisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa