Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wazazi Mkoani Geita kusimamia watoto na kuhakikisha wanakwenda shule na kuachana na tabia ya utoro kwani serikali imedhamiria kuwapatia elimu bora.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo leo tarehe 07 desemba, 2021 wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa 6 shule ya Sekondari Nyamigota kwa Tshs. Milioni 120 za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19.
"Nitoe wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wetu wanaenda shuleni waachane na utoro nasi tutachukua hatua kwa wazazi ambao watoto wao watakua watoro na walimu mfundishe kwa bidii." Mkuu wa Mkoa.
"Tumeondoa ujinga na maradhi na tunaona Mhe. Rais wa awamu ya sita amesema anataka watoto wote wapate elimu, hayo ni mapinduzi yanaendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita na ndio maana watoto 405 tunawapokea katika kata hii moja pekee ifikapo mwezi januari 2022," amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru kwa kujituma kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taifa."Sababu ya serikali kuboresha huduma zake kama umeme, barabara, Maji na Elimu ni kuwataka wananchi wake wajiletee maendeleo, Miaka 60 ya Uhuru si wakati wa kulala usingizi na si wakati wa kubweteka hivyo tutumie fursa, Usalama na amani ya nchi ni wakati wa kujituma na kujiletea maendeleo hivyo tutimize wajibu wetu." Amesema.
Vilevile, Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua Ujenzi wa Madarasa kwenye shule ya Sekondari Lutozo na Shantamine pamoja na kupanda miti ambapo ameagiza Ukamilishaji wa kazi ndogo ndogo zilizobakia na utunzwaji wa miti iliyopandwa. "Hatua mliyofikia ni hatua ya matumanini kwani kazi zilizobaki ni ndogo na tutafanikisha tarehe 15 Disemba, 2021 aliyoagiza waziri wa TAMISEMl tutakamilisha."
"Kupanda mti sio kazi kazi ni kuitunza, nawaomba muitunze miti hii kwani miti inaleta uhai, miti inaleta mvua na hewa safi na kila mmoja aitunze kama kumbukumbu ya miaka 60 ya Uhuru, tukumbuke kuwa wanaopanda miti ni wachache lakkini wanaotumia kunufaika nayo ni wengi." Mhe. Senyamule.
"Miaka 60 ya Uhuru na 59 ya Jamhuri, nchi hii iko salama na tunaishi kwa upendo na hii ndio Tanzania iliyoundwa na wazee wetu na usione vyaelea ujue imeundwa, na hapa nataka niwaambie wazazi wote kuwa Serikali itaendelea kutoa Elimu Bure nchini." Amesema Ndugu Ally Rajab Kwa niaba ya CCM wilaya ya Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inatekeleza ujenzi wa madarasa 347 ya Sekondari na 5 kwenye shule shikizi na kufanya jumla ya Madarasa 352 chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Uviko 19 kwa Jumla ya Tshs. Bilioni 6.9.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa