• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC na RAS Geita Wajitambulisha kwa Watumishi Wilayani Geita, Wasisitiza Kuinua Uchumi.

Posted on: August 11th, 2022

Na Boazi Mazigo-Geita

Zikiwa zimesalia siku 12 kufikia zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, Mkuu wa Mkoa Geita Mhe.Martin Shigela pamoja na Katibu Tawala Mkoa Geita Prof.Godius Kahyarara wamefanya ziara ya kikazi kujitambulisha kwa uongozi na watumishi wa Wilaya za Mkoa wa Geita wakianzia Wilaya ya Geita Agosti 10, 2022.

Akiongea akiwa Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Geita, RC Shigela amesema, anamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kuona kuwa yeye anaweza kumsaidia kazi kwenye Mkoa wa Geita lakini pia amemshukuru kwa fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa mkoani Geita. Vilevile, amezipongeza halmashauri za wilaya ya Geita kwa ukusanyaji wa mapato uliyovuka malengo kwa zaidi ya asilimia 100 kwa mwaka wa fedha 2021/22 huku akisisitiza mambo mbalimbali kwa watumishi wa umma.

RC.Shigela amesema, “kwakuwa mimi na RAS tumeteuliwa siku moja, tumeona ni bora leo tuambatane kwenye utambulisho na kisha baadaye kila mmoja atapata nafasi ya kuendelea na ratiba yake. Kikubwa kutoka kwenu niombe muwe wabunifu katika kuongeza mapato, wanaokusanya mapato wahakikishe fedha zinapelekwa benki kabla ya kutumiwa, mshirikiane, mpendane, mfuuate sheria, taratibu na kanuni za nchi, msimamie vyema miradi ya maendeleo, pelekeni asilimia 40 ya mapato yenu kwa wananchi, epukeni makundi, jueni yakuwa Mhe.Rais anatupenda sana na anategemea mageuzi makubwa sana kutoka kwetu”

Akimaliza, RC Shigela amesema kuwa, iko haja ya kuimarisha na kuhuisha vikao vya mashauriano ya mpango wa matumizi ya fedha zinazotokana na wajibu wa Kampuni kwa Jamii CSR kutoka Mgodi wa GGM ili Mkoa ushiriki kikamilifu lakini vilevile kuwa na mpango utakaowezesha mapema mwaka wa fedha unapoanza, mikataba iwe imesainiwa na utaratibu uanze mara moja.

Naye Katibu Tawala Mkoa Geita Prof.Godius Kahyarara akiwa Geita TC na Geita DC amesema, “nimshukuru Mhe.Rais kwa kuuniteua ma kunileta Geita, hivyo basi kama watumishi tunayo kazi ya kubuni vyanzo vipya vya mapato na tuongeze ajira kwa vijana, kubwa zaidi tuchangie kwenye pato la taifa kupitia makusanyo na kodi. Yatupasa kufikia mwaka 2025 tuifikie asilimia 30 ya uuzaji mazao nje ya nchi kwakuwa hadi sasa mazao yanayoongoza ni Dhahabu na Mchele na bahati nzuri yote yanapatikana Geita, na hapo ndipo tutaipata tafsiri halisi ya kaulimbiu yetu “Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima, lengo likiwa ni kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Nao Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.Wilson Shimo, Wabunge wa Majimbo ya Geita Mhe.Kanyasu John Constantine, Mhe.Mhandisi Tumaini Magesa Pamoja na Mhe.Joseph Kasheku Musukuma wamesema, wanamshukuru Mhe.Rais kwa kuwateuwa viongozi hao RC na RAS na kwamba watwapa ushirikiano katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo.

RC na RAS Geita wanaendelea kujitambulisha kwenye Wilaya za Mkoa wa Geitta ambapo Agosti 11, 2022 watatembelea wilaya ya Mbogwe na Bukombe.

Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa.



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa