Na Boazi Mazigo – Geita.
Ikiwa ni saa chache baada kuhitimishwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan mkoani Geita, mkuu wa mkoa Geita mhe.Martine Shigela amekabidhi zawadi kwa makundi mbalimbali zilizotolewa na Mhe.Rais Samia akiwa ziarani mkoani Geita, ziara iliyodumu kwa siku mbili kuanzia tarehe 15 Oktoba, 2022.
Akizungumza wakati akikabidhi zawadi hizo Oktoba 16, 2022, Mhe.Shigela amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia moyo wake wa upendo kwa kufanya ziara mkoani Geita kwa kutembelea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, kuwasalimia wananchi katika eneo la Katoro-Buseresere, akazindua mradi wa Kituo cha Kupozea Umeme Mpomvu, kufungua Kiwanda cha kusafisha Dhahabu Geita Gold Refinery kinachomilikiwa na mtanzania na kisha kuwasalimia watanzania kupitia wananchi wa mkoa wa Geita katika uwanja wa CCM Kalangalala, ambapo Oktoba 16, 2022 Mhe.Rais alihitimisha ziara yake kwa kuwasalim wananchi katika eneo la Runzewe kata ya Uyovu Wilayani Bukombe na kisha kuendelea na ziara yake mkoani Kigoma.
“tumshukuru sana Mhe.Rais kwa msaada wa mablanketi,mashuka, sabuni, sukari, miswaki na dawa zake, pampas, chupa za chai, vikombe n.k. na ni matumaini yangu kwamba watoto waliokuwa wanahangaika kwenye namna ya kuishi ikiwemo kukosa hata nguo za kujifunika sasa wanaishi vizuri. Lakini pia niwapongeze viongozi na wadau wote kwa kufanikisha ziara hii” alisema Mhe.Shigela.
RC Shigela alimaliza kwa kutoa rai kwa vituo vinavyopokea zawadi hiyo kutoka kwa Mhe.Rais Samia kuhakikisha zinawafikia walengwa na kutumika kwa malengo kusudiwa na visigeuke kuwa bidhaa kuuzwa madukani, kwakuwa lengo la Mhe.Rais ni kuwasaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu wakiwemo yatima na kwa kufanya hivyo watoto watatambua kuwa Rais wao anawapenda, kuwajali na kuwathamini.
Akishukuru kwaniaba ya taasisi zinazojihusisha na kuwahudumia watoto yatima na waishio mazingira magumu, bi. Juliana Aloyse kutoka kituo cha kulelea watoto yatima Neema House amesema anamshukuru sana Mhe.Rais Samia kwa moyo wa upendo kwa kutoa msaada na zawadi kwao kama kiongozi wa nchi, akiahidi kuhakikisha zinawafikia walengwa akiwahasa pia taasisi aina yake zitakazopokea zawadi hizo kuzitumia kama yalivyo maelekezo ya Mhe.Rais kama yalivyotolewa na mkuu wa mkoa.
Naye katibu tawala mkoa Prof.Godius Kahyarara alisema, zawadi alizozitoa Mhe.Rais ametoa zawadi hizo kwa makundi hayo kwa mkoa mzima watu zaidi ya 3,211 wakiwemo watoto wa mahitaji maalum, yatima, nyumba za Masista, Mapadri, BAKWATA n.k
Hakika hii ndiyo Geita ya Samia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa