SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUJENGA VITUO VYA AFYA MKOANI GEITA
Serikali ya Mkoa wa Geita imesema inaendelea kushirikiana na wananchi kusogeza huduma za afya karibu na wanapoishi kwa kujenga na kuimarisha vituo vya kutolea huduma.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo kwa Mkoa wa Geita yamefanyika Wilaya ya Mbogwe, Mgeni rasmi Mhe. Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wauguzi na Sekta ya Afya kwa ujumla hivyo inaendelea kujenga na kuimarisha vituo vya kutolea huduma hizo kwa kushirikiana na wananchi ili wapate huduma hizo karibu na maeneo yao. “Serikali inaimarisha ubora wa huduma ya afya inayotolewa kwa wananchi kwa kuvipatia vituo hivyo vifaa vya uchunguzi na tiba, Pia inafanya jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa dawa za kutosha, rasilimali watu kama vile madaktari, wauguzi, wakunga na wataalam wengine wa Afya”.
Aidha, ametoa rai kwa wauguzi kwa kuwataka kubadilika na kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuzingatia viapo vyao licha ya changamaoto zilizopo. Hata hivyo,amezitaka Halmashauri za Wilaya Mkoani Geita zihakikishe kuwa ziwatekelezea wauguzi madai yao ya sare mapema iwezekanavyo pia kulipa madeni yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa