Serikali Mkoani Geita imekamata dawa za viuadudu 428 vilivyotakiwa kupelekwa kwa wakulima wa pamba vijijini badala yake vikapelekwa kwenye maduka ya kilimo kinyume na matarajio ya serikali.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu wadau wa zao la pamba walipokutana kujadili maendeleo ya kilimo hicho.
Akizungumza na wakurugenzi na wakuu wa idara wa Halmashauri za Mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amesema hadi sasa watuhumiwa 12 wanawashikiliwa na vyombo vya dora katika Halmashauri za Chato , Geita DC na Geita mji.
“Tumegundua viuadudu mia nne ishirini na nane(428) vilivyotakiwa viingie vijijini kwa wakulima vimeingia kwa mawakala kwenye maduka ya pembejeo kinyume na taratibu, mwongozo na mpango uliokusudiwa kwa hiyo watuhumiwa 12 tayari wamekamatwa katika Wilaya mbili, wilaya ya Chato tumepata viuadudu tisini na sita(96), Geita Mji tisini na nane (98)na kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita tumepata mia mbili thelasini na Nne(234)”Amesema Mkuu wa Mkoa.
Hata hivyo Mhandisi Robert Gabriel ameiagiza TAKUKURU pamoja na vyombo vya dola kuwakamata wote waliohusika na usambazaji wa dawa hizo vikiwemo na vikosi kazi ngazi ya kijiji kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa