TANAPA yafadhili ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, Ofisi na Boti ya Doria Wilayani Chato
Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhadhili Wilaya Chato ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.
Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi amesema mradi wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe, kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni 6.
Aidha Dkt. Kijazi amesema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya yenye thamani ya shilingimilioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutoka na ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ nikutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi ya kisiwa cha Rubondo ili pokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelani na kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa utasimamia vyema miradi hiyo. AidhaMkuu wa mkoa wa Geita amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusia uvuvi haramu. Ameagiza wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.
Bodi ya wadhamini ya TANAPA ipo mkoani Geita kwa ajili ya vikao vya bodi hiyo ambavyo vinafanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo. Wakiwa Wilayani Chato wajumbe wa bodi ya wadhamini ya TANAPA walipatafursa ya kutembelea uwanja wa ndege wa Chato ambapo wamesema kukamilika kwa uwanja huo utasaidia kuibua fursa nyingi za kiuchumi na kuongezeka kwa idadi ya watalii kufika hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na hifadhi zingine zilizo jirani hasa katika mkoa wa Kigoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa