Timu ya wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita imeendelea kuwasisitiza wahandisi kuwasimamia kwa ukaribu wakandarasi ili kuwa na kazi yenye matokeo na tija kwa wananchi ambao ni watumiaji na wanufaika wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara.
Hayo yameshauriwa kwa wataalam wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Bukombe Machi 31, 2022 baada ya timu hiyo ya mkoa kufika na kutembelea miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa wilayani Bukombe
Akiongea kwa nyakati tofauti, Bw.Last Lingson ambaye ni Afisa kutoka idara ya Mipango na Uratibu ambayo inahusika na uratibu wa ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na wataalam wengine (wakiwemo wahandisi) alisema, ni muhimu sana kuhakikisha wakandarasi wanasimamiwa kwa ukaribu ili kuepusha kuchelewesha miradi lakini pia kuhakikisha kazi inayokamilika inakua haina mapungufu kwa ustawi wa Maendeleo ya taifa.
"Wito wetu bado ni uleule, wahandisi endeleeni kuwasimamia wakandarasi kwa ukaribu kwani itawapunguzia changamoto nyingi zinazosababishwa na wakandarasi wawapo kazini. Lakini pia, tuwahimize wakandarasi walioongezewa muda kujitahidi kuutumia vyema muda huo ili kuwahisha huduma kwa wananchi". Alisema Bw. Lingson.
Kwa upande mwingine, wakandarasi waliokutwa eneo la kazi akiwemo LYAKALE Civil Works Co.Ltd na KASERKANDIS Construction & Transport Co. Ltd wameahidi kufanya kazi kwa bidii ukizingatia majira ya mvua ili hali hiyo isiwe kikwazo kukamilisha kazi kwa wakati.
Naye Bw. Eustance Mahuma, Fundi Sanifu Mkuu kutoka TARURA Bukombe alisema, wao wanaendelea kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi wote na watahakikisha masharti ya mkataba yanafuatwa na ushauri uliotolewa na wataalam wa ofisi ya mkuu wa mkoa utazingatiwa kwani yote ni katika kufanikisha shughuli za serikali kuwaletea Wananchi maendeleo.
Mvua zimeelezwa kuwa changamoto kukwamisha wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati, au pengine kuonekana wamechelewa, lakin hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika pamoja na hali iyo, kazi zinaendelea.
Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima.
Kazi Iendelee
Boazi Mazigo
Afisa Habari
Geita RS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa