Licha ya kuwa na hali ya mvua inayoendelea maeneo mbalimbali mkoani Geita, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Wilaya ya Chato wamesema kuwa wakandarasi bado wapo kazini na wanaendelea na kazi, lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati.
Hayo yameelezwa Aprili 1, 2022 na Meneja wa TARURA Wilaya ya Chato Mhandisi Daniel Mwiru wakati Timu ya wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita ilipofika wilayani humo kwa ajili ya kufuatilia miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA
Wakiongea wakati wa majumuisho baada ya kutembelea utekelezaji wa miradi, Timu ya Mkoa pamoja na TARURA Chato kwa pamoja wamesema, ni muhimu sana kutoa muda wa kutosha wa kumaliza kazi kwa mkandarasi kulingana na mazingira, ukitolewa mfano wa mvua zinazonyesha, maeneo yenye chemchem ambazo zimekuwa zikichelewesha miradi.
kwa upande mwingine,Bw. Last Lingson ambaye ni Afisa kutoka idara ya Mipango na Uratibu ambayo inahusika na Uratibu wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na wataalam wengine (wakiwemo wahandisi) aliendelea kusisitiza kuwa ni muhimu sana kuhakikisha wakandarasi wanasimamiwa kwa ukaribu ili kuepusha kuchelewesha miradi lakini pia kuhakikisha kazi inayokamilika inakua haina mapungufu kwa ustawi wa Maendeleo ya taifa.
Hata hivyo, Mhandisi Mwiru aliongeza kuwa, usimamizi unafanyika kwa ukaribu kama ambavyo timu hiyo imeshuhudia kuwa kazi zinaendelea na mkandarasi yupo kazini lakini pia wao wamejipanga kulinda miundombinu kwanza kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia sheria zao, kisha kwa makubaliano wataweza kuitunza miundombinu. Vilevile, alisema kuwa, wao ni mashuhuda kwa jinsi fedha za tozo zilivyosaidia eneo kubwa
"tumejipanga na tayari tumekubaliana na wananchi kuwa, watakaa wenyewe na kukubaliana kutengeneza njia za kupitisha mifugo kwa miezi miwili na nusu kuanzia Aprili 1,2022 na kwa sehemu watakazohitaji kuvusha mifugo tutakubaliana tutaweka alama. Baada ya zoezi hilo, tutaanza kutumia sheria kutoa adhabu (faini) lengo kwa pamoja tuilinde miundombinu kwani zimetuia fedha nyingi kuijenga" alimaliza Mhandisi Mwiru.
Miradi ya Barabara iliyotembelewa ni pamoja na Matengenezo ya Muda Maalum Barabara ya Nyamirembe-Kazunguti ya urefu wa Km 2.2, Matengenezo ya Kawaida Barabara ya Nyabirezi-Kachwamba urefu wa Km 4.0, Matengenezo ya Muda Maalum Barabara ya Chabulongo-Nyang’homango urefu wa Km 3.3 zote za kiwango cha changarawe na katika hatua mbalimbali za matengenezo na Ujenzi wa Barabara ya Old CRDB kiwango cha Lami urefu wa Km 0.8 ambayo inaendelea kujengwa.
Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima. Kazi Iendelee.
Boazi Mazigo
Afisa Habari
Geita RS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa