Na Boazi Mazigo-Geita RS
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Geita imehitimisha ziara yake kwenye wilaya zote tano za mkoa wa geita kwa kutembelea na kuona miradi mbalimbali ya sekta ya Elimu, Maji na Utawala katika Halmashauri ya wilaya Nyang'hwale na kueleza kufurahishwa kwao juu ya usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo hadi kutamani mkoa wote kuwa na maendeleo yanayofanana kwa maana ya utekelezaji na usimamiaji mzuri wa miradi.
Hayo yameelezwa Agosti 27, 2023 wakati wajumbe hao walipokuwa kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Busengwa kupitia mradi wa BOOST iliyoletewa shilingi milioni mia tano arobaini na laki tatu (540,300,000)
Akiongea akiwa kwenye miradi tofauti tofauti, mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema,"nimpongeze Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi akiwajali wananchi, lakini pia nyang'hwale nawapongeza sana kwa usimamizi mzuri wa miradi. Natamani mkoa wetu uwe na maendeleo yanayofanana na tuisimamie vizuri. Lakini pia, hakikisheni mnasimamia malipo ili vibarua kwakuwa wengi wamekuwa wakidhurumiwa. Hata hivyo niwapongeze viongozi wenu kuanzia mkuu wa wilaya, katibu tawala, Mkurugenzi na wataalam, mnafanya vizuri"
Mwenyekiti Kasendamila alimaliza kwa kumpongeza mwakilishi wa Mkuu wa mkoa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Geita kwa kusimamia vizuri maandalizi ya ziara hayo pamoja na wataalam wa ofisi ya mkoa huku akiwasihi watumishi wote kudumisha upendo, mawasiliano na mahuasiano mema.
Kwa upande wake Mhe.Cornel Magembe,mkuu wa wilaya ya Geita na mwakilishi wa mkuu wa mkoa geita alisema, anawashukuru wajumbe wote wa kamati hiyo ambayo imepita wilaya zote na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.
Akiongea kwaniaba ya viongozi wenzake, mkuu wa wilaya Nyang'hwale Mhe.Grace Kingalame amewashukuru kamati hiyo pamoja na viongozi wa serikali kwa kutembelea miradi wilyani humo akisema " huku ndiyo kutekeleza falsafa ya CCM kwa kutekeleza Ilani yake" kisha kuahidi kuzingatia ushauri wote uliotolewa na kuufanyia kazi.
Ziara wilayani Nyang'hwale imehitimishwa kupitia miradi yenye gharama ya jumla ya Bilioni 8,561,053,035,5.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa