Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Machi 30, 2020 ametangaza Juma la maombi maalumu ya Kuliombea Taifa kwa Mwenyezi Mungu kutuepusha na janga la Ugonjwa hatari wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona na yatahitimishwa Jumapili ya Tarehe 05, April 2020 ambapo Viongozi wa Madhehebu ya dini watakutana kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji (GEDECO) kwa Dua na Sala.
Wakati huohuo, Mkoa wa Geita waunda kikosi kazi Maalum kupambana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu Covid 19 unaosababishwa na Virus vya Corona ambapo Mganga Mkuu wa Mkoa atawaongoza Wajumbe kumi na tano wanakotoka sekta mbalimbali Mkoani hapa huku Afisa Afya Mkoa atakua Katibu.
Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa Japhet Simeo amewasihi viongozi wa Madhehebu ya Dini kuelimisha Jamii juu ya Kubadili tabia na kuhakikisha wananawa mikono mara kwa mara, kuepuka kukaa sehemu zenye misonamano na kutakasa mikono wanaposafiri ili kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa huo.
“Twendeni tukatoe elimu ya kupambana na Ugonjwa huu, tusirudi nyuma kwenye hili na Mungu baba atawasimamia”. Alisema Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Aidha, Askofu Stephano Saguda kwa niaba ya Madhehebu ya dini ya Kikristo alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wao kama wakristo watahakikisha Jamii inapata Elimu waliyopewa na Mganga Mkuu na kwamba wataitoa kila mara wanapokutana na waumini wao.
Wakati huohuo, Shekhe Kabaju kwa niaba ya Waislamu Mkoa wa Geita alimshukuru Mkuu wa Mkoa na akamuahidi kuwa elimu walioipata kwenye wito huo ni jambo jema kwa Maisha ya wananchi wa Geita na kwamba atahakikisha anaifikisha kwenye misikiti yote ili waumini waipate kwa wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa