Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel alipofanya ziara ya kushtukiza na kujionea uzalishaji wa dhahabu katika Elution Plant (viwanda vya kuchomea Carbon zenye Dhahabu) mjini Geita.
Mhe. Mhanidisi Gabriel amefurahishwa na muitikio wa wamiliki wa elution plant hizo kuongezeka siku hadi siku ambapo ametembelea eneo la Nyanza lililoko Mbugani Mjini Geita lenye viwanda hivyo saba na kujifunza mengi ikiwemo jinsi dhahabu hiyo inavyopatikana.
Mkuu wa Mkoa ameshuhudia dhahabu yenye uzito wa Kilogramu moja na gramu mia mbili (Kg. 1.2) yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Mia Moja (Tshs.100, 000,000/=) ndani ya dakika arobaini na tano (45) alizofika kwenye Elution Plant moja ya Mwananyanzala, hali iliyompelekea kusema;
“ninadhani mmeona wenyewe, carbon za kilo mia nne mteja wa kwanza, mia nne mteja wa pili tumepata kiasi hiki cha dhahabu, hii ni dalili njema kwa Mkoa na hizi ni kutoka Elution moja tena kwa dakika hizo, sasa vipi kwa Elution nyingine?. Ninataka fedha inayopatikana kwenye dhahabu irudi kwa jamii, ijenge miundombinu lakini pia wafanya biashara wa Dhahabu njooni tuna Elution saba hapa Nyanza eneo la Mbugani, hazina mzigo zinawasubiri mlete carbon lakini pia Kamera za usalama zipo (CCTV Camera), hakuna haja ya kuogopa na Mkoa uko shwari hakuna tatizo, Elution nyingine zinaendelea kujengwa ,gesi na transfoma za kutosheleza mahitaji yenu tumekwishazipokea shaka ondoa sasa” alisisitiza.
Moja ya wateja kutoka Nyarugusu Wilayani Geita (jina limehifadhiwa), alishukuru kwa namna ambavyo serikali inavyohusika kuanzia hatua ya kwanza anaweka mzigo wake hadi hatua ya upimaji kwani kwa kufanya hivyo hata yeye anaona hakuna nafasi ambayo ataibiwa mzigo wake na kumpongeza Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla kwa jitihada anazoendela kuzifanya pamoja na wasaidizi wake kwa kuwa yeye kama mteja na Serikali ndiyo huweka makufuli kwenye mitambo ya kuchomea dhahabu hivyo hana hofu ya kuibiwa kama zamani.
Kwa upande wake moja ya wamiliki wa kiwanda cha Jema Africa, Elution Plant iliyokuwa ikifanya shughuli zake Mkoani Mwanza amesema, “kwakweli ninaziona faida za kuja Geita, wateja ni wengi, tofauti na nilivyokuwa kule, hivyobasi nawaita wateja waje tu ulinzi upo, Geita ni amani kazi zinaendelea”.
Kuelekea Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita, watanzania na wageni mnaalikwa kushiriki jukwaa hilo litakalofanyika kuanzia tahere 15-16.08.2018 linaloratibiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na MKoa wa Geita ambapo mtaweza kushuhudia bidhaa zinazozalishwa Mkoani Geita lakini pia Maonesho Makubwa ya Teknolojia ya Dhahabu yatakayofanyika kuanzia tarehe 24-29 Mwezi Septemba, 2018.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa