• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

Posted on: May 2nd, 2025

Wafanyakazi wa Taasisi za Umma pamoja na zile za binafsi katika Mkoa wa Geita wamepewa rai ya kuhamasishana ili kila mmoja aboreshe taarifa zake katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la wapiga kura, zoezi ambalo limeanza tarehe Mosi mwezi Mei na kumalizika tarehe 7 Mei 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Martine Shigela ametoa rai hiyo tarehe 01 Mei 2025 alipokuwa akizungumza na hadhara ya watumishi wa Mkoa wa Geita wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala Manispaa ya Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita amefafanua kuwa wafanyakazi wakiboresha taarifa zao watapata fursa ya kuchagua viongozi ambao wana sera za kuwasaidia wafanyakazi katika changamoto zinazowakabili, pamoja na kuwapima viongozi waliokuwa madarakani awali na wametia nia ya kuendelea jinsi walivyowasaidia watumishi wao walipokuwa madarakani.

Mhe. Shigela ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia Mkoa wa Geita fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali zikiwemo Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ameeleza kuwa Serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 7.7 kwa ajili ya kulipa madai na malimbikizo ya mishahara, likizo na masaa ya ziada kwa watumishi wa Umma Mkoani Geita kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Kadhalika Mkuu wa Mkoa wa Geita ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuridhia kutoa fedha hiyo ili kuondoa malalamiko na kutengeneza mazingira rafiki ya wafanyakazi wakiwa Ofisini na nje ya ofisi. Pamoja   na kuupatia Mkoa wa Geita watumishi wapya 8,424 kati yao 6,202 wakiwa ni walimu.

Maadhimisho ya Mei Mosi yalikwenda sambamba na tukio la Mkoa wa Geita kugawa pikipiki 20 kwa Maafisa Tarafa wa Mkoa mzima ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuwarahisishia utendaji kazi Maafisa hao. Pikipiki hizo zimenunuliwa kwa gharama ya shilingi Milioni 75,306,000

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wote, Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Geita Ndg. Magilu Ndebile Kabengwe ametoa ombi kwa Serikali kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi ikiwa ni pamoja na baadhi ya waajiri kusuasua  kuwasilisha michango ya watumishi hasa wa Sekta binafsi, ucheleweshaji wa malipo ya likizo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara nk.

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka na kutambua jitihada zilizofanywa na wafanyakazi walioandamana kupigania haki za wafanyakazi Duniani, kwa mwaka 2025 Maadhimisho hayo yaliongozwa na Kauli Mbiu isemayo “ Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki.”

Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Wafanyakazi Geita Wapewa Rai Kuboresha Taarifa Zao

    May 02, 2025
  • Waziri Mavunde Aaagiza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nyuma Ya CSR Geita

    April 15, 2025
  • Mabonanza ya Watumishi Yawe Endelevu - DC Kingalame

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa