Na Boazi Mazigo – Geita RS
Viongozi ngazi za wilaya wameendelea kusisitizwa kuwamasasisha wananchi mkoani hapa kujihadhari na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwa ni kipindi cha mvua za Vuli kama ilivyohimizwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA.
Wito huo umetolewa Oktoba 20, 2023 kwa wajumbe wa kamati ya wataalam ya mkoa ya usimamizi wa maafa na kusisitizwa juu ya kuwaelimisha wananchi lakini pia kuendelea kukutana na kamati ngazi za halmashauri, kata na vijiji ili kujengeana uwezo wa namna ya kukabiliana na majanga pindi yatakapotokea.
Akiongea kabla, wakati na baada ya kikao hicho, Dkt.Omari Sukari ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo na kaimu katibu tawala mkoa alisema, kila taasisi inao wajibu wa kujipanga kwenye eneo lake lakini pia ni muhimu kuwa na mpango wa tahadhari na kwamba baada ya wao kukamilisha mipango yao, itawezesha uwepo wa mpango wa tahadhari wa mkoa ambao umebeba maeneo yote.
“kwanza niwapongeze kwa kikao hiki, lakini pia nitoe wito mnaporudi kwenye maeneo yenu, mkasisitize utoaji wa elimu kwa wananchi ili wachukue tahadhari kwani huu ni wajibu wetu. Lakini si hivyo tu, mkashirikishane kupitia vikao, ili muwe na uelewa wa pamoja”, alisema Dkt.Sukari.
Dkt.Sukari alimaliza kwa kusisitiza kuwa kila mmoja anayo nafasi katika kupunguza athari ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa mvua za vuli, hivyo kuwataka wajumbe hao kuwa tayari muda wote kuanzia wakati huu.
Kwa upande wao na kwa nyakati tofauti, wajumbe wa kamati hiyo wakiwemo kutoka jeshi la polisi, la akiba, zimamoto na uokoaji, na viongozi wa taasisi nyingine wamesema wapo tayari na wamejiandaa kibajeti lakini pia hata kuwa tayari kurejesha miundombinu ambayo inaweza haribiwa kama vyanzo vya maji, nguzo za umeme, madaraja, barabara n.k
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa