Jumla ya washiriki 193 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wamepewa mafunzo ya uandikishaji wa CHF Iliyoboreshwa (Mfuko wa Afya ya Jamii uliyoboreshwa) kati ya 586 ya jumla ya watakaoendelea kupata mafunzo katika maeneo mengine ndani ya Mkoa wa Geita. Mafunzo yameandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Tuimarishe Afya (Health Promotion and System Strengthening - HPSS) unaofadhiliwa na Shirika la MaendeleonaUshirikano la Uswisi (SDC).
Akifunga mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika Katika shule ya sekondari Katoro, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewashukuru mradi wa HPSS wanaoendesha mafunzo huku akiwapongeza washiriki waliohudhuria amewataka washiriki hao kwenda kufanya kazi kama walivyoelekezwa huku akiwasihi kuwa waaminifu, akiwahahakikishia uwepo wa serikali ya mkoa kwa ajili yao wanapopata changamoto.
Amesema, “washiriki kumbukeni mmepewa heshima na jukumu kubwa mnatakiwa kulitendea haki, mpango mliopewa ni mkubwa. Pia niwapongeze HPSS kwa kuja Geita, tulikuwa na changamoto ya mpango huu, lakini tunashukuru maombi yetu kujibiwa kupitia ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa, ili kuhakikisha jamii ya mkoa wa Geita inakuwa na afya njema ili iweze kuzalisha”.
Mhandisi Gabriel ameendelea kutoa wito kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuitikia mpango huu kutokana na faida ulizo nazo zikiwemo uwezo wa kutibiwa mahali popote ndani ya mkoa kwa kufuata taratibu, kasha akakabidhi vifaa vya kazi kwa washiriki hao.
Akisoma taarifa ya mafunzo, Bi Fiona Chilunda, Mshauri Mtaalamu Mradi wa Tuimarishe Afya kutoka Dodoma na Msimamizi wa Mafunzo Mkoa wa Geita amesema wameanza mafunzo hayo kuanzia tarehe 17 - 22 Disemba 2018 na yamejumuisha Maafisa Usimamizi wa CHF Iliyoboreshwa wa mikoa, wilaya na kata lakini pia Maafisa Uandikishaji 3,700 wa mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, SimiyunaTabora. Gharama yake ni Shilingi 30,000/= kwa mwaka ikiwa na faida mbalimbali ikiwemo kuhudumia wategemezi 6 na kwamba kila mmoja atapata kadi yake, atatibiwa kwenye vituo vya kutolea huduma ndani ya mkoa kwa rufaa lakini vilevile kwa mikoa ya nje kwenye mikoa ambapo tayari mradi huo unatekelezwa
Bi. Chilunda amesema, Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo Maafisa Uandikishaji kutumia mfumo wa kidigitali kuandikisha wanachama wa CHF akisema kuwa awali CHF Iliyoboreshwa imekuwa ikitekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Shinyanga kutokea mwaka 2012. Kutokana na kufanya vizuri kwa kuandikisha jumla ya kaya 338,209 (Dodoma 156,921, Morogoro kaya 111,523 na Shinyanga kaya 69,765), ndipo OR-TAMISEMI wakauchukua ili utekelezwe na Serikali.
Ameendelea kusema kuwa, waandikishaji ni wnanchi walioaminiwa na maeneo wanapotoka wakiwemo mawakala wa malipo kwa mtandao kama Tigo pesa, M-Pesa, n.k
Awali, Mganga Mkuu MKoa, Dkt. Japhet Simeo alisema kuwa CHF hii imeboreshwa na kwamba kila dmtegemezi ataweza kutibiwa kwa kuonesha kitambulisho chake tofauti na zamani ambapo kitambulisho kimoja tu ndicho kilikuwa kikitumiwa na wategemezi wote. Pia ameshukuru serikali ya Tanzania na wadau wa mradi wa HPSS kwakuwa kila kaya inayoandikishwa kwa Tsh. 30,000 mwandikishaji atapata asilimia 10 ya ile fedha na hiyo ndiyo itakua malipo yake kwa kila mwaka atakapokuwa akiandikisha.
Hivyo kwa kiasi kikubwa kutakua na salio la kuwezesha kuboresha miundombinu, kununua dawa na kihakikisha waateja wote waliojiandikisha wanapata huduma.
Washiriki, wao aliahidi kufanya vizuri katika zoezi hilo la kuhamasisha na kusajili wananchi ili watumie CHF Iliyoboreshwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa