Na Boazi Mazigo-Geita RS
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Geita imeendelea kuwapa wananchi tabasamu kwa kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake pale ilipotoa kauli kwa wataalam wote wanaosimamia ujenzi pamoja na malipo kuhakikisha vibarua wanalipwa, watu ambao wamekuwa wakidhurumiwa na mafundi jambo ambalo limekuwa likiwakosesha haki mafundi wengi.
Akiongea mbele ya watendaji, watumishi wa umma na wajumbe wa kamati anayoiongoza alipokuwa wilayani Chato Agosti 24, 2023, mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita Nicholaus Kasendamila alisema, " watendaji, kumekua na tabia ya mafundi kudhulumu fedha za vibarua wao, Sasa mnapowalipa hakikisheni mnasimamia na vibarua wanaowadai mafundi hao ili nao walipwe. Haipendezi wao wanalipwa halafu wao hawawalipi vibarua wao. Hivyo tabia hii isiwepo kwenye mkoa huu"
Agizo hilo limetokana na changamoto hiyo kukutwa kwenye baadhi ya miradi inayoendelea na kwakuwa vibarua hao huingia mikataba na mafundi, hivyo wao hukosa namna ya kujua ni lini fundi kalipwa ili nao waweze kupata ujira wao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa