NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS TAMISEMI AFUNGUA OFISI ZA KANDA YA MAGHARIBI MFUKO WA LAPF MKOANI GEITA
Mkoa wa Geita umepata neema ya kupata Ofisi ya Kanda ya Magharibi baada ya mfuko wa LAPF kuzindua Ofisi zake za Kanda ya Magharibi itakayohudumia mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Akihutubia wakazi wa Mji wa Geita katika viwanja vya mfuko huo mkoani hapa mgeni rasmi, Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi amewapongeza LAPF kwa kuona umuhimu wa kufungua Ofisi za Kanda mkoani hapa kwani itakuwa msaada kwa watumishi wa Mkoa huu na mingine kwakuwa walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Amewashukuru kwa kujali wateja wao mpaka kufikia mtumishi anapata mafao kabla ya kustaafu, na kutoa huduma zingine za uzazi ambazo zinawapa unafuu wa kupata mahitaji muhimu baada ya kujifungua. Ameikata mifuko mingine kuiga mfano huu ili kubaini na kukabiliana na kero mbalimbali za watumishi. Katika hatua nyingine amezitaka Halmashauri za Wilaya zote nchi kuhakikisha kuwa zinapeleka michango ya wanachama katika.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF Bwana Eliud Sanga amemkabidhi madawati 100 kwa Naibu Waziri wa Tamisemi ukiwa ni mchango wa taasisi hiyo kwa LAPF ambayo hata hivyo yameelekezwa katika shule ya Sekondari Nyantorotoro iliyopo Halmashauri ya Mji Geita.
Vile vile Mheshimiwa Naibu Waziri ametumia ziara hiyo kukagua ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami ya Katundu hadi eneo la Amerikani Chips yenye urefu wa Kilometa 2.6.Amemuagiza Mkandarasi kuhakikisha barabara hiyo inakabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa ifikapo January 30/2018.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa