• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wiki ya Unyonyeshaji Duniani Mwaka 2019 Geita Kuwezesha Wazazi Kufanikisha Unyonyeshaji

Posted on: August 2nd, 2019

Mkoa wa geita umezindua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa mwaka 2019, ambapo miongoni mwa malengo ya wiki hii yamejikikita katika kuinua uelewa wa jamii kuhusu usawa wa kijinsia, sheria zinazowezesha kulinda, kuendeleza, na kusaidia unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuboresha lishe ya watoto na jamii.

Uzinduzi huo umemefanyika Agosti 2, 2019 katika eneo la kituo cha afya Katoro kilichopo  mamlaka ya mji mdogo katoro, halmashauri ya wilaya ya geita, ambapo mgeni rasmi Bw. Vunza Mohamed kwaniaba ya Mganga mkuu wa mkoa, katika hotuba yake ameeleza imani aliyonayo kwa wadau mbalimbali wa lishe na waandishi wa habari kutumia ujuzi na taaluma walionayo kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu utunzaji wa ustawi wa watoto hasa wale wachanga na wadogo kwani ni jukumu la kila mmoja na kuwashukuru wadau wa Mradi wa USAID Boresha Afya kwa kuwa wadau muhimu kwenye utekelezaji wa maadhimisho ya wiki hii.

Amesema, “kwakuwa wiki hii huadhimishwa kila mwaka tangu mwaka 1992, ni vyema sasa tuungane kwa pamoja katika kukumbushana umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha unyonyeshaji maziwa ya mama kama njia bora zaidi ya kujenga afya ya mama na mtoto kimwili na kiakili”

Bw. Mohamed amesisitiza kuwa, bado takwimu za unyonyeshaji za mkoa zipo chini licha ya kuwepo kwa elimu mbalimbali za unyonyeshaji wa maziwa ya mama kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na wahudumu wa afya ngazi ya jamii, kwani ni asilimia 71 tu ya watoto wenye umri chini ya miezi sita wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee wakati asilimia 40.7 wakiendelea kunyonyeshwa maziwa ya mama mpaka wanapofikisha umri wa miezi 24, kisha kukata utepe ishara ya kuzindua wiki hii.

Akikagua banda la lishe, Bw.Mohamed amewasisitiza akina mama kuhakikisha mtoto mchanga wa umri chini ya miezi sita anakunywa maziwa ya mama pekee na si vyakula vya kawaida ili kuijenga lishe yake kuepuka udumavu.

Kwa upande wake Bw.James Katto ambaye ni mwakilishi wa mratibu Mradi wa USAID Boresha Afya Mkoa wa Geita amesema, wao wanaungana na wadau wa lishe nchini na nchi nyingine duniani kuadhimisha wiki hii wakijua kuwa, maadhimisho haya yamelenga kusisitiza juu ya umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji maziwa ya mama.

Bw.Katto ameendelea kusema, tafiti za kidemografia za mwaka 2015/16 zinaonesha kwamba, asilimia 38.9 ya watoto chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Geita wamedumaa, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha kitaifa ambapo ni asilimia 31.8, udumavu unaochangiwa na lishe duni kipindi cha ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili. “Hivyobasi katika maadhimisho ya wiki hii, Mradi USAD Boresha Afya utawezesha watoa huduma katika vituo vya afya kutoa elimu ya lishe, kutathimini hali ya lishe ya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano na kutoa ushauri wa afya na lishe kwenye jamii” alimaliza Bw.Katto.

Hivyo, wito umetolewa kwa wananchi wote mkoani Geita kutumia fursa hii muhimu ya wiki ya unyonyeshaji kufika katika vituo vya afya kupata ushauri wa kitaalam kuhusu afya na lishe kwa ujumla na kutambua hali yao ya lishe.

Akitoa neno la shukrani, mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya geita dkt.Raphael Mhana, amewashukuru wadau wa mradi wa USAID Boresha Afya huku akiwasihi akinamama kuhakikisha wanaiandaa afya ya mtoto mapema kwani inaanza kabla ya kubebwa ujauzito na hata baada ya mtoto kuzaliwa basi wahakikishe mtoto ananyonya maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza bila kupewa chakula kingine.

Kwa mwaka 2019, Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani yameanza Agosti 1, 2019 na yatakamilika Agosti 7, 2019 na kwa mkoa wa Geita yatafanyika kwenye halmashauri zote kupitia vituo vya kutolea huduma za afya.

Ni muhimu wanajamii kupewa taarifa sahihi ili kuwasaidia wanawake wote waweze kunyonyesha na kuwatunza watoto wetu ili hatimaye tupate taifa lenye watu bora zaidi.



Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa