• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mamlaka za Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Baraza la Wafanyakazi Geita Lamuenzi Baba wa Taifa kwa Kusaini Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi, RC Gabriel Ahimiza Mshikamano

Posted on: October 13th, 2020

Katika kuuenzi mchango wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baraza la wafanyakazi mkoa wa Geita limetia saini Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi uliohusisha Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) pamoja na Sekretarieti ya Mkoa wa Geita  jumanne ya Oktoba 13, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Akifungua kikao cha baraza hilo, mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa, anaiamini timu ya sekretarieti ya mkoa na kwamba itatekeleza mkataba huo kwa ufanisi na ubunifu huku akihimiza mshikamano, kuombeana na kuhurumiana kwani binadamu hukosea.

“mimi ni shemasi wa mkoa huu, ninawaomba watumishi tushikamane, tuhurumiane, tuombeane na tusameheane kwani kukwazana ni sehemu ya maisha”

Mhandisi Gabriel alimaliza kwa kusema kuwa analo deni kubwa kwa watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Geita kwani tangu amekuwa Kiongozi ndani ya mkoa huu, hajawahi kukwazana na mtumishi yeyote hivyo kujiona ana deni la kuwalipa watumishi hao kwa wema wao kwake, kisha kufungua kikao hicho.

Kwa upande wake Ndg.Mgasa Chimola ambaye ni katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) amesema, anaushukuru uongozi wa mkoa kwa maandalizi ya kikao hicho muhimu kuwezesha utiaji saini mkataba huo, jambo ambalo linaonesha msisitizo wa dhana ya ushirikishwaji na mshikamano na kwamba wao kama TUGHE wapo tayari kutoa ushirikiano kwa ofisi ya mkoa katika kuhakikisha wafanyakazi wanazingatia haki na wajibu.

Mganga mkuu wa mkoa Dkt. Japhet Simeo hakuwa mbali kuwasilisha mada inayohusu lishe na kuhimiza watumishi kuzingatia namna bora ya ulaji ikiwa ni utekelezaji wa kampeni iliyoanzishwa na katibu tawala mkoa wa Geita ndg. Denis Bandisa ya kutoa mada mbalimbali kwenye vikao mbalimbali zikiwemo mada kuhusu rushwa, afya, namna ya kujiaandaa kustaafu, ujasiriamali n.k

Akiahirisha kikao hicho, mwenyekiti ambaye pia ni katibu tawala mkoa wa Geita ndg. Denis Bandisa amesema kuwa, watumishi ni vyema kujitahidi kufanya kazi kwa bidii na si kuangalia namna ya kupata vyeo huku akisema, “tujifunze kusikiliza na visivyo tufurahisha” kwa lengo la kuwa tayari kupata elimu ya ziada kisha kuwashukuru wajumbe wa kikao kwa kushiriki na kwa pamoja kuazimia kukutana kwa ajili ya kikao kingine kabla ya maandalizi ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Vikao vya baraza la wafanyakazi hufanyika kufuatia Agizo Na.1 la mwaka 1970 lililotolewa rasmi tarehe 10/2/1970 na Hayati Mwl.Julius Nyerere kupitia dhana ya ushirikishwaji ambayo ni uundwaji wa mabaraza na ili kuweka mkazo, likaimarishwa na Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 na Kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108, Sheria ya Majadiliano Katika Utumishi wa Umma Na.19 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2017.

Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka -2021, Mkoa wa Geita. December 18, 2020
  • Fomu ya Ushiriki Kwenye Maonesho ya Tenkolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mjini Geita August 06, 2019
  • Vigezo vya Udhamini, Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji Kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita August 06, 2019
  • Matokeo Darasa la Nne Mkoa wa Geita January 11, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Robert Gabriel aagiza kukamatwa kwa Mtendaji wa Kijiji aliyetoroka na fedha za Michango ya Madawati

    February 03, 2021
  • RC Geita Aipa Joto la Ushindi Timu ya Geita Gold FC Dhidi ya Pamba Sports Club ya Mwanza, Asema ana Deni Kwao.

    November 20, 2020
  • "Walimu na CWT, Tuisaidie Jamii Ijue Tulipotoka, Tulipo na Tunapokwenda" RC Geita Anena Hayo

    October 17, 2020
  • Wataalam wa Ardhi Watega Sikio Kupata Tafsiri ya Ardhi Waliyonayo Wananchi Mkoani Geita

    October 17, 2020
  • Tazama Zote

Video

Mwaliko Jukwaa la Fursa za Biashara Mkoani Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: Box 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa