Lengo la Kitengo hiki ni Kutoa utaalamu na huduma katika habari, mawasiliano na mazungumzo
na umma na vyombo vya habari. Majukumu ya Kitengo hiki ni kama yafuatayo;-
(i) Kuzalisha na kusambaza nyaraka kama vile vipeperushi, makala na
majarida kuhabarisha umma juu ya shughuli zinazofanywa na Mkoa.
(ii) Kuratibu taarifa kwa waandishi wa habari kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
(iii) Kushiriki katika mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala yanayohusu
Mkoa.
(jv) Kuhuisha taarifa za Mkoa kwenye tovuti.
(v) Kuwezesha utoaji wa taarifa na mawasiliano kuhusu jamii na
shughuli za maendeleo ya kiuchumi.
(vi) Kuhamasisha na kuratibu vyombo vya habari ili kuwasiliana na wadau pamoja na
umma kwa ujumla kuhusu shughuli za kimkakati zilizopangwa na Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa