Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigela amesema kuwa mradi mkubwa wa Maji Unaotekelezwa kwenye chanzo chake Katika Kijiji Cha Senga Halmashauri ya Wilaya ya Geita utaanza kutoa huduma ya maji ya uhakika mwezi wa Kumi na Mbili baada ya mradi huo kukamilika
Mhe. Martine Shigela ameyasema hayo alipokuwa akikagua utekelezaji wa mradi huo katika Kijiji Cha Senga Oktoba 18,2025
Mkuu wa Mkoa wa Geita ameongeza kuwa Mkandarasi wa mradi huo ametoa maelezo yanayoridhisha na kuwahakikishia wananchi kuwa Mwezi Disemba 2025 Mradi utakuwa tayari kutoa huduma ya maji safi na salama kwa Wananchi.
Mhe.Shigela amefafanua kuwa mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa unaogharimu zaidi ya Bilioni 144 wenye kuzalisha zaidi ya Lita milioni na kujaza matenki Ili kuhakikisha upatikani wa Maji safi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Geita muda wote.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe.Hashim Komba ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mradi wa Maji kwa Wananchi wa Wilaya ya Geita na kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi na salama kwa urahisi.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi Wa mazingira (GEUWASA) Mhandisi Frank Changawa amesema Mradi wa Maji unaotekelezwa katika miji 28 una matenki mawili yenye jumla ya Lita milioni tano na yote yamekamilika,na kuahidi kusimamia mradi huu kikamilifu ili ifikapo Mwezi Disemba 2025 uanze kuhudumia Wananchi kwa kuwapatia maji safi na salama
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Senga Paul Benjamin Isaka ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan na kuhaidi kuwa mradi utalindwa na kutunzwa Ili kutimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha Wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama jirani na makazi yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa