Lengo kuu la Seksheni hii ni Kukuza maendeleo na utoaji wa huduma za afya, hatua za kinga,
ustawi wa jamii na lishe kwa Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
(i) Kuratibu na kushauri kuhusu utekelezaji wa sera za afya katika Mkoa.
(ii) Kuratibu upangaji na utekelezaji wa huduma za afya, ustawi wa jamii na
usafi wa mazingira katika Mkoa.
(iii) Kuratibu usimamizi wa vituo vya afya katika Mkoa.
(iv) Kufuatilia na kutathmini usimamizi wa huduma za afya zinazotolewa na Vituo vya kutolea huduma za afya vya umma
na binafsi katika Mkoa.
(v) Kutoa msaada wa kujenga uwezo kwa Halmashauri katika utoaji wa huduma za afya.
(vi) Kushauri RS na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya maandalizi na kukuza uwezo wa kupambana
mlipuko wa maradhi.
(vii) Kutoa ushauri kuhusu shughuli za VVU/UKIMWI katika Mkoa.
(viii) Kukuza ushiriki wa jamii juu ya matumizi ya bima ya afya.
(ix) Kutoa msaada wa kupambana na magonjwa ya milipuko yanapotokea katika Mkoa.
(x) Kuratibu na kuhuisha data za afya, ustawi wa jamii na lishe
kwa Halmashauri.
(xi) Kutoa msaada wa kitaalamu kuhusu afua za lishe kwa Mamlakaza Serikali za Mitaa.
(xii) Kuratibu huduma za afya ya kinga.
(xiii) Kuwezesha na kuratibu masuala ya mazingira na usafi wa mazingira katika Mkoa.
(xiv) Kuratibu upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na
vifaa vya kutolea huduma za afya katika Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa